Wednesday, February 26, 2020

UPWEKE USIKUINGIZE KWENYE MAHUSIANO:


Kuna baadhi ya watu wanaingia kwenye, kwasababu ya hali ya upweke waliyonayo katika maisha, hali inayopelekea kupoteza muda wao na hata kuumizwa pasipo kutarajia.
πŸ‘‰Unapolazimisha mahusiano eti kwasababu ya upweke basi kubali kuwa mtumwa wa mapenzi, Utatumika mno pasipokutarajia, utajikuta unatumia pesa nyingi na hata kupoteza muda wako kwa mtu usie na malengo nae.
πŸ‘‰Kuna wakati unasema acha nijishikize kwa mtu Fulani kwasababu nipo mpweke, Acha nitumie hela yangu ili nipate mademu niondokane na upweke au acha nitumie mwili wangu ili nipate masela wanifariji niondokane na upweke, Upweke unakuingiza kwenye mambo ambayo sio matarajio.
πŸ‘‰Unapoteza muda wako mwingi kudate na mtu kwa kuigiza, yan upo nae tuu Ili siku ziende, sio kwaajili ya misingi ya maisha ya baadae, Uhusiano wa aina hiyo unaweza kukupa jeraha ambalo hukulitarajia.
πŸ‘‰Kukutana kwenu kutakuwa hakuna faida, maana hakuna mwenye ukweli juu ya mwenzie, huenda mwanamke utaempata ukizan ni mkeo mtarajiwa kumbe yupo kwako kwaajili ya kukuchuna tuu au mwanaume uliempata ukizan ni mmeo mtarajiwa kumbe hana mpango na ww yupo kwako sababu ya upweke na kujilidhisha kingono.
πŸ‘‰Yafanye mahusiaho yawe preparation ya ndoa yako, Ingia kwenye mahusiano ukiwa tayari na misingi dhahit ya maisha kwamba yes sahiv nahitaji mke au nahitaji mume ili tujenge maisha.
πŸ‘‰Lakin usifanye mahusiano kuwa starehe za ujanani, utadate na wanaume au wanawake wangapi sababu ya upweke, ni nin kinakufanya mpaka uwe mpweke. Jee ni kweli huna marafiki ambao unaweza kufanya nao kazi, mkachallenge na upweke Ukaondoka.
πŸ‘‰Mwili wa mwenzio sio sehemu ya kumaliza upweke wako, Wala pesa za mwenzio sio sehemu sahihi ya kumaliza upweke wako ebu pambana tafuta marafiki wachapa kazi ili uende nao sambamba kwajili ya kujenga maisha yako.
πŸ‘‰Ukiendekeza upweke wa kihisia utajikuta unaishi maisha ya kutumiwa, na kutumika bila mpangilio wala msimamo wako. Jitathimini na ufanye maamuzi ya haraka.
J4REAL


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/upweke-usikuingize-kwenye-mahusiano.html

No comments:

Post a Comment