Wednesday, February 26, 2020

KATIKA NDOA MUME AMEAGIZWA UPENDO, MKE AMEAGIZWA UTII:


πŸ‘‹Katika patanisho la watu wawili yaan mwanaume na mwanamke ili wawe mke na mume. Imeandikwa mke ana amtii mumewe na mume ampende mkewe.
πŸ‘‰Mume aliyeagizwa upendo ni yupi? Kwann mungu asimuagize mwanaume utii, Bali akamuagiza upendo. Mwanaume ni kichwa cha familia sharti asimamie mambo yote na kuna utii ndani ya upendo wa mwanaume.
πŸ‘‰Kuna baadhi ya wanaume wanadhani swala LA upendo au upendo unaoongelewa ni ule wa maneno kwamba utamwambia mkeo I love u au nakupenda basi hapo ndio umeonyesha upendo kwa mkeo noo.
Upendo tunaouzungumzia ni ule wa vitendo.
πŸ‘‰Unafahamu fika mwanamke ni ubavu wako inamaana usipompenda hata ww hujipendi, Upendo wa vitendo ndio unaotakiwa kuonyesha kwa mkeo kwamba ana tatizo hili na hili onyesha kumjali na kumpenda kama ubavu wako, Kwann unahudumia watu wa nje na mkeo haumjali je ni upendo gani unaojivunia kwake.
πŸ‘‰Naelewa unawaza namna gani ukiona mkeo hakutii, mkeo hakueshim unawaza ni jinsi gan umefanya mpaka anakudharau, Ila usiache kumpenda we mpende tuu mungu atamrejesha kwenye njia sahihi Tu.
πŸ‘‰Mke aliyeagizwa utiifu ni yupi? Je kwann mungu hakumuagiza mwanamke upendo Bali akamuagiza Utii. Mungu pekee anajua mwanamke amejawa upendo ila anajisahau katika utiifu, ndio maana akampa jukumu LA utiifu kwa mumewe.
πŸ‘‰Kuna baadhi ya wanawake wanadhani tukiongelea utiifu basi ni woga au kujishusha thamani. Nataka niwaambie hivi kumtii mumeo sio kumuogopa, Bali ni kuonyesha thamani yako kwamba namuheshimu na kutimiza agano la mungu. Unaona haya gani kujishusha kwa mumeo, huyo si ndio aliwekwa kama kichwa cha familia yako.
πŸ‘‰Wapendwa wanawake mliojaliwa ndoa nawasisitizia upendo. Na mwenyeenzi mungu awajalie kutambua na kutekeleza agano lenu juu ya waume zenu ili ndoa zenu zipate kudumu. Mtii mumeo naye atakupenda
πŸ‘‰Najua ni maumivu gani ambayo yanampata mwanamke asiyeona upendo wa mumewe kwake. Najua unaumia vipi ukiona mmeo hakupendi lakin usiache kumtii mungu atamrejesha kwenye mstari Tu.
πŸ‘‹Mungu awaongoze kuishi katika UPENDO na UTII.
J4REAL
Image may contain: 4 people, people standing, wedding and outdoor


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/katika-ndoa-mume-ameagizwa-upendo-mke.html

No comments:

Post a Comment