πUsitake kila mtu aishi kwaajili ya kukufurahisha au kukupa furaha.
πUsitake kumfurahisha kila mtu, wapendeze wale wanaopendezwa nawe.
πUsitake kupendwa wala kusifiwa na kila mtu, Penda pale unapopendwa.
πUsitake watu wote wapende unachofanya au wafanye unachopenda.
πChunga sana Sio kila kinachokuumiza wew basi na wengine kitawauma, unaweza ukawaeleza wakakuongezea maumivu.
πFuraha ndogo uliyo nayo Imeushibisha moyo wako, usitake furaha kubwa zaidi kwa watu wasio na umuhimu kwako.
πSilaha kubwa ya kuitunza furaha ya moyo wako ni wew kuishi sawa sawa na aina ya mazingira uliyopo, usitake kuwageuza watu vile wanavyoishi.
J4REAL
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/misingi-ya-kuilinda-furaha-yako.html
No comments:
Post a Comment