>>Maisha yako ni kama nyota, dhababu, mbao au nguo. Kuna wakati unaweza kuona kwamba labda hili jambo naweza kuliepuka lakin utaona haliepukiki kwasababu inakupasa na ni lazima wewe upite hapo.
>>Hakuna shortcut ya nyota kung'aa bila kuchomoza kizani, hakuna shortcut ya dhahabu kung'ara bila kupita kwenye moto, wala mbao haiwezi kunyooka tuu bila kurandwa, pia nguo haijakamilika kama haijapita kwenye machine.
>>Kuna muda unafika katika safari yako ya maisha unajikuta ni lazima kabisa upite hapo unapopita ili mambo yako yanyooke na hata ukijaribu shortcut unajikuta unafeli lazima utarudi tuu kwenye mstari wa lazima.
>>Wakat mwingine unaweza kuona umeachwa, unaweza kuona dunia imekuegemea, waweza kuona uko peke yako lakin kumbuka ni lazima upite hapo unapopita ili ung'ae tuu, Kitu ambacho kinakua na ulazima ni kitu ambacho hakiepukiki.
>>Haitajalisha unaumia kiasi gani, haitajalisha unapata maumivu na uchungu kiasi gani, haitajalisha umeelemewa kiasi gani wala haitajalisha umechoka kiasi gani lakin itakulazimu kupita tuu hapo ili ufikie lengo.
>>Kuna wakati maisha yako yanakuwa kama NYOTA, unapita kwenye wimbi zito la majaribu, misukosuko ya kimaisha, vikwazo na kila aina ya mikasa lakini ni lazima upambane uchomoze kwenye hilo Giza ili ung'ae.
>>Kuna wakati maisha yako yanakuwa kama DHAHABU unapita kwenye wakati mgumu kiasi kwamba unaona jamii imekuegemea, unaonekana mbaya kwa kila mtu, maneno ya kashfa na kejeli yanasemwa juu yako lakin ni lazima uvumilie ili ufikie kusudi. Wacha wakuunguze tuu lakin ndio kung'aa huko.
>>Kuna wakati maisha yako yanakua kama MBAO, unapita kwenye randa randa za maisha watu wanajaribu kukukwamisha, watu wanajitahidi kukukwaza kila unachojaribu watu wanakukatisha tamaa na kukuvunja moyo lakini usijali randa inapopita kwenye mbao lazma ikwame kwame ndipo inyooke. Hata wewe mbali na vikwazo vyote unavyokutana navyo katikati ya safari usiogope mambo yako yatanyoolka tuu.
>>Kuna wakati maisha yako yanakuwa kama NGUO, unaishi na watu wenye kukuhukumu muda wote, maneno mengi yanasemwa juu yako yanakichoma kama sindano, watu wanakanyaga mafanikio yako lakin jua hivi nguo bila kutobolewa na sindano haijakamilika. Hivyo wacha wakusem
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/nikikwambia-maisha-yako-ni-kama-dhahabu.html
No comments:
Post a Comment