Monday, February 24, 2020

MAANA YA NENO TUNAENDANA NA UHALISIA WAKE👩‍❤️‍👨


Mapenzi yaliyo na wawili waliopendana kwa dhati ni kama watu wawili "MAPACHA"
Maana ya neno KUENDANA ni sawa na MAPACHA kwamba ni kweli kila mmoja ana tofauti na mwenzie lakini WANAFANANA KWA 95%
Yaani ukitaka kujua wewe na Mwenza wako mnaendana basi tafuta UWIANO WA KI TABIA NA MATENDO walau kwa asilimia 60 Kwani mmezaliwa tofauti na malezi ni tofauti, Ila UPENDO 💘 unakuja kuwaweka pamoja na kuwa kitu kimoja walau maana ya MNAENDANA iwe kwa sehemu kubwa.
Mapenzi ya sasa yameghubikwa na TAMAA kila mmoja kutaka kupata anachokiwazia, na hapo ndipo utanielewa kwamba WENGI HAWAENDANI KI TABIA NA KI MATENDO ila wanalazimishana kupelekana wakiamini katika MABADILIKO lakini tabia ya mtu ni kama NGOZI ni ngumu kuibadili ikiwa amekulia kwenye malezi hayo🤔
Usiingie kwenye MAHUSIANO/NDOA na Mtu ambaye UMEMPENDA ila yapo mambo hayaendi Sawa ukitegemea mbele ya safari utaweza kumbadilisha
Tafuta Mtu ambaye ANAENDANA na wewe hata kama hujampenda kwa kiwango Kikubwa, Kwani ni rahisi kujifunza KUMPENDA MTU ambaye VIGEZO na masharti amezingatia😂😂
Maana usipokuwa mjuzi wa kubaini haya Mpaka mnazeeka ninyi ni watu wa MIGOGORO TU.
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria 🔨


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/maana-ya-neno-tunaendana-na-uhalisia.html

No comments:

Post a Comment