πMaisha yako yanaweza kupoteza muelekeo ghafla pindi utakapoanzisha mahusiano au kuoa.
πMaisha yako yanaweza kuyumba kiuchumi pindi utakapoanzisha mahusiano au kuoa.
πHaijalishi una nguvu kiasi gani kwenye uchumi na elimu, lakin nguvu hizo zitaathiriwa ghafla na aina ya mwanamke utakaye ishi nae.
πUtasoma sana, Utakua na pesa nyingi, Elimu yako na Uchumi wako vitakufanya uonekana mpumbavu na mjinga kutokana na aina ya maisha utakayo yachagua.
πSuala la kuoa ni suala la kutafakari kwa mapana sio kukurupuka, Unavyooa unaongeza mtu kwenye maisha yako hivyo hivyo mtu huyo anatakiwa aongeze kitu kwenye maisha yako.
πSio unaingia kwenye mahusiano unafilisika, au unaoa unaanguka kiuchumi elimu yako inakuwa haina msaada kwenye maisha yako.
πHaijalishi mwanamke utakayemuoa atakuwa vipi labda hana elimu wala kipato lakini akiwa akili ya kufikiri kwa upana juu ya maisha yenu basi anaweza akaongeza utajiri wa mawazo kwako.
πUsipende mwanamke wa kusema YES kwa kila utakachoamua, huyo mwanamke atakupotezea muelekeo, mpende mwanamke anaekupa challenge penda mwananke anayekukosoa.
J4REAL
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanaume-chunga-sana-hili-elimu-na.html
No comments:
Post a Comment