“Shemeji naomba nikuambie kitu, sema chonde chonde naomba usimuambie Eliza kwani akijua ni mimi nimekuambia atanichukia milele. Lakini nimekuambia kwakua nakuonea huruma, kuoa mwanamke ambaye hazai inaniuma sana.
Hata kama ni mimi ningekuambia mwanzoni kabisa wa mahusiano. Jane aliongea kwa wasiwasi kidogo akimuangalia shemeji yake, alikua akimzungumzia rafiki yake Eliza ambaye walianza urafiki tangu wakiwa kidato cha tano mpaka walipomaliza chuo na sasa wanafanya kazi shemu moja.
Alex alimsikiliza kwa makini kutaka kujua kisa kizima. “Unamaanisha nini kusema kuwa hazai sikuelewi…” Aliulza Alex na hapo ndipo Jane alianza kujimwaga na kutiririka, kila kitu kuhusu rafiki yake ambaye ilikua imebaki wiki mbili tu kufunga ndoa.
“Najua hajakuambia kwani ungekua ushamuacha, ila wakati tukiwa kidato cha tano, Liz aliumwa sana. Alikua na uvimbe kwenye kizazi hivyo kuathiri bleed yake, sasa walimfanyia upasuaji na uvimbe ulikua mkubwa hivyo wakamtoa kizazi.
Hawezi kuzaa na ni watu wachache sana wanajua, mimi najua kwakua ndiyo msiri wake, nimekuambia wewe kwakua nakuonea huruma. Tafadhali usinielewe vibaya shem ila kama angekua anakupenda basi angekuambia…”
Kabla ya kumaliza hata kuongea Alex alinyanyuka kwa hasira alipiga meza teke na vinywaji vyote kumwagika, aliingia kwenye gari na kuondoka. Jane alibaki anashangaa huku akitabasamu akijua kuwa rafiki yake anaenda kuachwa na wote wanabakia usela kuendelea kudanga tu.
****
Maandalizi ya harusi yaliendelea, Alex hakumuambia chochote mchumba wake. Kitendo kila kilimuumiza sana Jane kwani alijua kuwa baada ya zile taraifa labda Alex angeahirisha harusi, lakini alistuka akijua kuwa Alex hajamuambia Liz kwani kama angemuambia basi angemnunia ila Liz aliendelea kumchangamkia kama rafiki.
Maandalizi ya harusi yaliendelea, Alex hakumuambia chochote mchumba wake. Kitendo kila kilimuumiza sana Jane kwani alijua kuwa baada ya zile taraifa labda Alex angeahirisha harusi, lakini alistuka akijua kuwa Alex hajamuambia Liz kwani kama angemuambia basi angemnunia ila Liz aliendelea kumchangamkia kama rafiki.
Kuona hakuna kinachoendelea Jane alimfuata Dada yake na Alex akamuambia ile kitu akimuambia kua ndugu yake kalogwa ndiyo maana hafanyi chochote. Dada yake naye alienda kwa Mama yake na wote Alex akaitwa kikao, Alex aliwaambia ameshajua hivyo anajua chakufanya.
Wote walikaa kimya wakisubiri labda alex ana hasira ya kudanganywa muda mrefu hivyo atamkataa mpenzi wake kanisani na kumuaibisha. Mama yake alijaribu kumsihi kuwa nibora kuvunja uchumba kuliko kumdhalilisha binti wa watu kwa kumkataa kanisani.
Alex aligoma kuongea chochote akisema yale ni maamuzi yake aachwe na maisha yake kwani yeye anajua kitu chakufanya. Mchana wakati wa ndoa mambo yalienda vizuri, watu waliojua walishangaa kuona hajamkataa kanisani na wote walikua na furaha, bado hawakujua nia ya Alex kuwa mkimya vile ilikua nini.
******
Usiku wakati wa sherehe, baada ya zawadi kutolewa, muda mchache kabla ya chakula, Alex aliomba kuongea. Tayari kulishakua na minong’ono na ndugu zake walipoona kachukua mike waliinama chini kwa aibu wakijua kuwa ndiyo alikua anamdhalilisha mke wake.
Usiku wakati wa sherehe, baada ya zawadi kutolewa, muda mchache kabla ya chakula, Alex aliomba kuongea. Tayari kulishakua na minong’ono na ndugu zake walipoona kachukua mike waliinama chini kwa aibu wakijua kuwa ndiyo alikua anamdhalilisha mke wake.
Alimuomba DJ kucheza CD moja, ilikua inaonyesha picha za Eliza tangu akiwa mdogo, zilienda mpaka pale akiwa hospitalini kipindi hicho akiwa ndiyo anafanyiwa upasuaji. Kila mtu alishangaa, wazazi wa Eliza walishikwa na butwaa, Mama yake alianza kulia. Eliza alibaki nawasiwasi kwani hakujua kilichokua kinaendelea.
“Najua wote mnashangaa, lakini kuna kitu nataka niongee. Miaka kama kumi iliyopita mke wangu alipata ugonjwa wa ajabu, si kitu amcho nilitaka kukizungumzia lakini kuna jambo limetokea hivyo nimeona nizungumzie.
Aliumwa akiwa na uvuimbe katika kizazi, baada ya kufanyiwa upasuaji wake ili kuokoa maisha yake walilazimika kutoa kizazi chake na aliambiwa kuwa hatakuja kuzaa tena. Wakati nakutana naye, siku ya kwanza tu aliniambia amenipenda ila hataki mahusiano na mimi kwani yeye hawezi kuzaa.
Nilimuuliza kwanini akaniambia kila kitu, lakini nilimuambia kila siku mapenzi ya Mungu nilazima yatimizwe. Kama Mungu akisema hataki tuwe na watoto basi hata kama ungekua na kizazi mpaka cha pua usinge zaa lakini kama akisema kuwa utazaa hata kama ukikatwa kiwiliwili ukabaki na kichwa tu basi utazaa.
Nilimuambia nampenda yeye na si vingine. Alinikubali kwa shingo upande. Lakini kama nilivyosema kuwa Mungu ni wa ajabu, akisema jambo liwe basi linakua, mwezi uliopita alianzakujisikia vibaya, alipoenda hosipitalini alipata habari ambazo hatukuzitegemea.
Aliambiwa ana ujauzito wa miezi miwili, wote tulishangaa na tulivyomuelezea Daktari hata yeye alishangaa,. Ilibidi kufanyiwa vipimo vingine na kuona kua kumbe madakttari ambao walimtoa kizazi kipindi hicho walikosea na walitoa tu uvimbe na upande mmoja wa mirija ya uzazi.
Sasa wote leo mmenipa zawadi, ila Mungu kanipa zawadi kubwa zaidi, aliongea huku akitoa picha ya ya ultra sound ikionyesha picha ya ,mtoto wake akiwa na miezi minne tumboni. Kila mtu alilia kwa furaha, hakuna aliyeamini, Jane ambaye alikua pale aliinama chini kwa aibu.
Eliza hakuweza hata kusimama alikaa chini na kulia tu, Alex alimfuata na kumkumbatia huku akimuambia nakupenda. Sherehe iliendelea vizuri mpaka ikaisha, wakaingia kwenye gari kwenda kula honeymoon huku Eliza akiwa haamini kilichotpokea.
*****
Kufika tu chumbani Eliza alitaka kujua kwanini alidanaganya kwani hakukua na kitu chochote kilichotokea, hakuwa na mimba, nikweli alimuambia tangu siku ya kwanza lakini hakukua na miujiza yoyote. Alex alitabsamu na kumuambia.
Kufika tu chumbani Eliza alitaka kujua kwanini alidanaganya kwani hakukua na kitu chochote kilichotokea, hakuwa na mimba, nikweli alimuambia tangu siku ya kwanza lakini hakukua na miujiza yoyote. Alex alitabsamu na kumuambia.
“Ndugu zangu walishajua, kuna mtu aliwaambia hivyo waliniitisha kikao. Ingawa mimi nakupenda sana na sijali kuhusu mtoto lakini najua nguvu ya ndugu, watakusumbua sana na hutakua na amani. Hii ndiyo njia pekee ya kuwanyamazisha midomo ili ndoa yetu iwe na amani, najua baada ya hapa hawataongea tena na wale wanafiki watazdi kuumia.”
Aliongea kwa kujiamini, Eliza alimuelewa lakini bado alikua na wasiwasi. Alimuuliza, sasa miezi tisa ikifika sijifungui itakuaje. “Mungu ameleta watoto wengi duniani, kuna ambao amewaleta na kuwanyang’anya wazazi lakini sisi ametuleta kama wazazi ila akatunyang’anya watoto.
Sasa ikikaribia miezi tisa tutatafuta mtoto yatima mchanga na tutamlea kama wetu, najua hata asipofanana na mimi kwakua tatizo unalo wewe basi hakutakua na kelele. Lakini pia kwani kila mtu anayebeba mimba nilazima azae, hivi ikafika miezi tisa nikakupeleka Nairobi kujifungua.
Huko mtoto akafia tumboni nikasema tumezika huko huko nani ataniuliza, wakati huohuo tukitafuta mwingine? Nimeshafikiria kila kitu mke wangu, kwa sasa nataka tu nikufaidi sitaki kelele za watu, tutawaza daraja tukiufikia mto.
Eliza alipumua kwa nguvu alienda na kumkalia mumewe mapajani kisha akamuambia nina swali moja tu limebaki. Ile picha uliitoa wapi?” Alex alicheka na kumuambia “Ndiyo maana Mungu alileta wazungu kwaajili ya mambo kama haya, nili Google tu na ku print hata sijui nimtoto wa nani?”
Wote walicheka na kukumbatiana wakaanza kufanya yao, wakisubiri kuwaza daraja wakiufikia mto.
*****MWISHO
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/simulizi-shemeji-naomba-nikuambie-kitu.html
No comments:
Post a Comment