Saturday, February 1, 2020

KILA MMOJA NI MZURI ILA KUNA KITU KINACHOMFANYA MWENZAKO AKUONE WA THAMANI NA BORA KWAKE,NACHO NI MVUTO WAKO KWAKE.


Mvuto hautokani na muonekano wako wa nje ila ni vile unavyomfanya mwenza wako afurahi na kuona fahari kuwa na wewe.
Mvuto ni namna unavyojua kucheza na mapungufu ya mwenza wako na kumfanya akuone bora, ni vile unavyokuwa mbunifu kwake na kumfanya ajihisi ana bahati kuwa na wewe.
Mvuto ni zaidi ya sura na umbile, mvuto ni jumla ya tabia na matendo yako kwa mwenza wako, vile unavyomfanya mwenza wako azidi kuwa na hamu na shauku na wewe ndivyo mvuto wako kwake unavyozidi kuwa mkubwa.
Umbile lako linaweza kuwa namba 8 au sura kama imechorwa, ila kama humpi furaha na raha mwenza wako, huna mvuto kwake.
Wapo tunaosema wana sura mbaya ila inashangaza watu namna wanavyobabaikiwa na wapenzi wao, usishangae maana wana mvuto, wanajua nini wenza wao wanataka, nini wanakosa kisha wanakuwa suluhisho.
Mvuto wako unaanzia katika weaknesses za mwenza wako na namna anavyotamani, kama mwenza wako hupenda mwanamke mwenye kuvaa hijabu na mpole, hata uwe na sura ya malaika na umbile la mdoli, umepoteza mvuto kwake....!!!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kila-mmoja-ni-mzuri-ila-kuna-kitu.html

No comments:

Post a Comment