Saturday, February 1, 2020

WANAUME HATA WANAWAKE IKIWAPENDEZA MNAWEZA KUICHUKUA HII....!


Kuna wakati unaombwa na kijana ooooh sijui kutongoza nisaidie.
Duuuuh sipendi maombi Dizain hiyo.
Mimi naamini hakuna njia ya kumpata mwanamke isipokuwa ni ubunifu wako na kuzisoma alama zake za nyakati.
Ujue nini anakipenda,nini ukimfanyia hachoki kukukumbuka.
Tengeneza njia ili yeye akuingie sio wewe umuingie ili hali hana cha kushawishika kwako.
Wala sio kwa pesa,kupoteza pesa ili kumpata mwanamke ni matumizi mabovu ya pesa ni uvivu wa kutengeneza njia,tumia pesa ukimpata sio kumshawishi kwa pesa.
Wengi wanalia,mchawi pesa kumbee analiwa na asipate jibu la ndio,kesho,kesho kutwa miezi inakatika na usimpate.
Pesa imepotea ujaambulia kitu.
Tumia pesa baada ya yes,na kuwe na afya sio bora nakupenda.
Ukijua njia mwanamke anaipenda utaenjoy saana na ufanye mpango utakaeona anafaa oa fasta utulie na wako.
Hakuna njia moja ya kufika Ubungo.
Unaweza kupita njia yoyote ukaingia Ubungo,haijalishi umetumia muda gani.
Hata kwa kumpata mwanamke anaekuvutia.
Tengeneza ukaribu nae,usiwe na papara.
Kila mwanamke ana kaugonjwa kake kwa mwanaume,wanapenda ucheshi,wanapenda usimart,wanapenda mikogo ya kutembea,uongeaji,kila haina ya ulivyo kuna mwanamke mgonjwa,,sio pesa huyu wa pesa utajuana nae mwenyewe.
Yote kwa yote usjiumize,usijitese bure kulazimisha penzi kwa mwanamke hata chembe ya yeye kukufikiria hana,,utakuwa chizi buure.
Kila mtu na mtu wake,wewe angalia wa taype yako,wa kufanana na wewe.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/wanaume-hata-wanawake-ikiwapendeza.html

No comments:

Post a Comment