Saturday, February 1, 2020

WAPENDWA NATAKA TUFANYE JARIBIO MOJA MATATA SANA HAPA😎 NAANZA NA WANAUME!


Wanaume fanyeni hivi.😊😊😊
Chukua movie yoyote ile romantic, iweke halafu kaa uangalie na mkeo.
Ikifika kipande cha mahaba(Kissing, hugging, kubembelezana, au kubebana hivi) jifanye umeguna "Mmmh mahaba motomoto, raha kweli".πŸ’–πŸ’–πŸ‘„πŸ’˜
I: Ukimuona mkeo anatabasamu, then akakukombatia.
Basi hongera sana bro, huwa unamuonyesha mahaba mkeo.
Hayo ndio maisha ya kuishi na mkeo.
II: Ukimuona na yeye kaguna halafu kajibu "Mh, hayo mambo yanakuaga kwenye movie tu".
Pole sana bro, jua hapo udhaifu ni wako.
Unaishi na mkeo kama dada yako, hapati mapenzi ambayo anastahili kupata kutoka kwako.
(Najua 99% wengi mtapata jibu hili la piliπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚)
Kesho yake mchana mtumie message, mwambie "Mke wangu kipenzi nakumiss. I hope unaendelea vizuri. Natamani nimalize kazi niwahi home tufurahi my love".
Hapa sasa ChiiiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ukifika home ukimkuta anatabasamu, na kukupokea kwa furaha.
Hongera, inaonekana huwa mnawasiliana na mnaitana kimahaba.
Ila ukimkuta kanuna halafu anakuuliza "Hii message ulikuwa unamtumia nani, ukakosea ukaituma kwangu???"😐😐😐
Au akiuliza "Leo kwani umeingiwa na nini? Unajua sikuelewi elewi"πŸ™„πŸ™„πŸ™„
Basi jua udhaifu wako huo, ndoa yenu haina mawasiliano mazuri.
Na wala huwa hauna muda mzuri na mkeo.
*********
WANAWAKE SASA!
Haya wanawake na nyie twende kaziπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Amka mapema, jisafishe mwili na kinywa.
Fanya usafi wa mazingira, andaa nguo za kuvaa mumeo, andaa chai na maji ya kuoga mumeo.
Kisha nenda kitandani, mpandie juu πŸ˜πŸ˜πŸ˜ mbusu huku unamuamsha kimahaba(Usiposukumizwa hongeraπŸ˜€, ukisukumizwa pole).
Muache akaoge, akimaliza jifanye unamsaidia kumvalisha shati (πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€Asipokuambia "Hebu acha" au "Hebu sogea huko" hongera, akikuambia pole)
Akitaka kuondoka kwenda kazini, muage vizuri, mkombatie halafu mbusu.
Ukiona hajakusukumiza, au hajakushangaa, au hajakuuliza "We leo umeingiwa na nini?", "Hivi kakufundisha nani?", basi hongera sana.
Ukiona amereact vibaya, basi jua hapo tatizo ni lako.
Hajayazoea maisha haya unayomuonyesha, amezoea ule ukali wako, vurugu zako.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
**********
Kwa wale mtakaopata reactions mbovu, basi kaeni chini na wenza wenu.
Waelezeni jinsi maisha ya ndoa yanavyotakiwa kuwa.
Waelezeni jinsi unavyopenda muishi, na ndoa idumu katika upendo, amani, na mahaba.
Ndoa ni nusu ya pepo, na sio sehemu ya mateso.
Haya test imeanza, nasubiri majibu😁😁😁


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/wapendwa-nataka-tufanye-jaribio-moja.html

No comments:

Post a Comment