Saturday, February 1, 2020

MWANAMKE ANAWEZA KUBEZWA,KUDHARAULIWA NA WANAUME 10 LAKINI AKIJITOKEZA MWANAUME 1 AKAMSIFU...HUMPA UJASIRI NA KUJIAMINI NA KUWATAMANISHA TENA WALE 10 WALIOMPONDA.



Image may contain: 1 person
Mwanamke huyo atajikuta ananywea, anakosa kujiamini, anashindwa kujikubali kwajinsi alivyo.
Lakini maneno machache tu ya kumsifia kutoka kinywani mwa mtu mmoja, yule ampendae kwa dhati, yanaweza kumfanya asahau yote hayo mabaya aliyowahi kuambiwa.

Na kujikuta akipata nguvu mpya na kumfanya ajiamini na kujikubali zaidi na kujiona mwenye thamani kubwa sana chini ya jua.

Mwanamke huyu huyu anaweza akasifiwa na watu 100, kuwa yeye mzuri, au kapendeza, au yuko hivi na vile.
Atajikubali, atajiona mzuri, atajipenda zaidi.

Lakini maneno machache tu ya kumponda, kutoka kinywani mwa yule anayempenda kwa dhati.
Yanaweza kumfanya awaone wale 100 wote waongo.
Atajishusha thamani, atakosa kujiamini, atakosa kujikubali kwa jinsi alivyo.
**********

Nafsi ya mwanamke ndogo sana, uwezo wake wa kujiamini ni mdogo sana.
Mwanaume anayejitambua ni yule anayemjenga mwanamke wake kihisia na kuongeza uwezo wake wa kujiamini, kujikubali, kujipenda, kwa kumpa maneno yenye kuboost confidence yake.
Na kumfanya ajione ana thamani kubwa sana chini ya jua.

#Muu_Mata

Image may contain: 1 person


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanamke-anaweza-kubezwakudharauliwa-na.html

No comments:

Post a Comment