Saturday, February 1, 2020

KUMBUKA SHUKRANI NI "PASSWORD"...

...
Chukua kalamu na Karatasi andika mambo yote mazuri ambayo Mume wako amewahi kufanya kwako na kwa watoto(Kama wapo) kuanzia siku ya kwanza mlipokutana......Hata kama sasa hivi amekukasirisha, au yupo kwa mchepuko au hamjaongea wiki nzima fanya ninachokuelekeza.....Yaandike kwa mtiririko kwa namba mfano;
1)Alinichumbia, akalipa mahari, akanioa
2)Amenipa watoto wazuri
3)Alinihudumia vizuri wakati wa ujauzito na kujifungua
4)Anahudumia familia
5)Alininunulia nguo Mwaka jana Krismas
6)Anajua kuomba msamaha akikosea
7)Ananiridhisha katika tendo la ndoa
8)Ananisaidiaga kulipa madeni yangu
9)Ndugu zangu wakiwa na shida anasaidia
10)Ananilinda ndugu zake wasininyanyase
11)Ananishirikisha mipango yake
12)Tumenunua viwanja akaandika majina yangu/ya Watoto
13)Anajitahidi kurudi nyumbani kila wiki kukaa na familia japo anafanya kazi mbali
14)Nikimkosea nikiomba msamaha ananisamehe
15)Aliniletea zawadi birthday yangu ya Mwaka 1998
16)..........
:
YAANDIKE YOTE UNAYOKUMBUKA HATA YAKIFIKA ELFU MOJA ANZA KUMSHUKURU MUNGU KWA LIMOJA BAADA YA LINGINE
#Itakusaidia kuona upande mwingine wa wema wake na utagundua mume wako sio mbaya hivyo unavyomuona sasa na utamuombea kwa bidii zaidi !


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kumbuka-shukrani-ni-password.html

No comments:

Post a Comment