Monday, February 3, 2020

FAIDA 6 KIAFYA ZA KUFANYA MAPENZI SALAMA.

Image result for Utamu wa Jirani
Kujamiiana ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu, ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa na mwenza ambae mnaridhishana katika tendo la ndoa.

Si hivyo tu bali tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule, lakini kuna faida zozote za kiafya za kufanya tendo hilo?

Zipo faida za kiafya zinazotokana na kujamiiana.

1. HULINDA MWILI DHIDI YA MAGONJWA YA MOYO.
Wanawake ambao hufika kileleni angalau kwa mara mbili kwa wiki kila wanapojamiiana, wana uwezekano mdogo sana wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale wasiofika kileleni.

2. HUONGEZA UKAKAMAVU WA MIFUPA.
Wanawake waliokoma kupata hedhi ambao pia hujamiiana angalau mara mbili kwa wiki wana kiwango kikubwa cha homoni ya oesrtogen mara mbili zaidi ya wale ambao hawajamiiani.

Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa Wanawake waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa ujulikanao kama osteoporosis.

3. HUPUNGUZA MAUMIVU.
Kufika kileleni wakati wa kujamiiana ni tiba ya maumivu homoni ya oxytonic inayotolew kwa wingi kabla na wakati wa kujamiiana pamoja na viasili vya endorphins hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipanda uso, baridi yabisi, pamoja na dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi.

4. HUONGEZA AFYA YA UPENDO.
Kujamiiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na kuongezeka kwa homoni ya oxytocin ambayo huleta mshikamano, uaminifu na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.

5. KUFANYA MAPENZI KUNAONGEZA UREMBO WA MWANAMKE.
Wanawake wanaojamiiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na ukweli kuwa kujamiiana huongeza homoni ya oesrtogen ambayo hufanya nywele za Wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kungaa.

6. UPUNGUZA UZITO NA KUMFANYA MTU KUWA NA AFYA NJEMA.
Kujamiiana ni mazoezi mazuri, wakati wa kujamiiana mapigo ya moyo huongezeka kutoka wastami 70/dakika Mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na mtu anaefanya mazoezi kwa kiwango cha juu.

Kujamiiana huchoma karibu 200 calories Sawa na kukimbia katika mashine ya tredmill, mwanamke anaefika kileleni huchoma calories 47 zaidi.

Kwa ambao mko single mnatakiwa kuwa double ili mpate faida hizo.πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/faida-6-kiafya-za-kufanya-mapenzi-salama.html

No comments:

Post a Comment