Sunday, February 2, 2020

Elimu na kazi haviwez kukufanya uwe MkE au MUME bora.


Kumekuwa na mawazo na imani miongon mwetu linapo fika suala la KUOA au KUOLEWA.
Watu wengi wanaamin kuwa ukiishi na mtu mwenye elimu ya juu na ana kaz au mfanya biashara bas ni rahis kuishi maisha ya raha au kupata maendeleo haraka ktk familia.
UKWELI ni kwamba
Ili upate mafanikio inatakiwa uwe ume mpata mwanaume au mwanamke mwenye akili ya maisha na moyo wa kujitoa kwa ajili yenu nyote .
Unaweza kuoa mwanamke msomi na mwenye kaz lakin pesa yake ikaishia kununua mavaz na urembo tu.. Yaan hana wazo kusema anunue hata mifuko 2 ya sementi.. Yeye anamin kwa kuwa ume muoa HVO wajibu wako peke yako mwanaume
Vile vile waweza olewa na mwanaume msomi mwenye kaz kama we lakin akaishia kukuachia majukum ya ndan na watoto huku yeye akilewa na kutafuta michepuko,kisa tu mkewe una kaz au biashara.
Lakin unaweza kuolewa au kuoa mtu uliye maid elimu ya darasan lakin yeye akawa msaada mkubwa ktk maisha yako kwa ushaur na kujitoa.Anaweza jibana kwa biashara ndogo ya kuuza mkaa akanunua mfuko wa sementi... Anaweza kuwa mtu wa kujitoa na kukupa iman kuwa SKU utafanikiwa.
Hivyo tunapo fikiria kuoa na kuolewa
Tusiangalie sana elimu au kaz ya mtu Bali tuangalie kama anafaa kushirik pamoja kuinua kipato cha familia kwa namna yoyote ile.
Elimu na pesa ni ziada tu
Kikubwa upendo na uaminifu


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/elimu-na-kazi-haviwez-kukufanya-uwe-mke.html

No comments:

Post a Comment