Saturday, February 1, 2020

HIVI NDIVYO WANAWAKE WENGI WANAVYOZIVUNJA NDOA ZAO BILA KUJUA


Unakuta Msichana anaolewa lakini WIKI YA KWANZA TU,anataka Msichana wa kazi wakati hana hata Mtoto mdogo.unataka msichana wa kazi wa nini??, huo ni uvivu tu.Lazima uwe MWANGALIFU,wewe umeolewa tu,unataka msichana wa kazi wa nini? Unaweza ukajitetea na kusema ni wakukusaidia kazi- KAZI ZIPI? Unaweza ukajitetea na kusema, "Aa! unajua ninachelewa sana kutoka kazini,angalau nikute mtu wa kupika" MIMI ninakuambia unaanza vibaya.Kama ndiyo kwanza umeolewa tu,unataka wa kumpikia chakula mume wako awe ni msichana wa kazi,basi unaanza vibaya.....
Wakati huo ndio saa ya kumtayarishia mume wako mapishi ambayo hajawahi kuona kwenye nyumba ya Baba na Mama yake! Akikaa mwenyewe huku anakula anasema ASANTE MUNGU kwa kunipa Mwanamke wa namna hii, kwa sababu hajawahi kuona chakula kizuri cha namna hiyo ulichompikia HATA HOTELIN HAJAWAHI KUKIPATA..
Lakini unaanza tu maisha ya ndoa na kumbandikia mume wako watu wa kumuhudumia,mimi nakuambia unaanza vibaya,huko unakoelekea na ndoa yako siko.
Wengine kwa kisingizio cha kuwa tayari kwenye ndoa basi unakuta mwanamke anaacha mbwembwe zote na nakshi za kimapenzi kwa mme wake, majina kama BABY, HUBBY, DARLING, HONEY, SWEET HEART, MY CHOCOLATE n. k hamna tena eti umri umekwenda ni mtu mzima sasa hivyo hawezi fanya mbwembwe za kitoto. Mme anarudi kazini anakukuta unanuka jasho na maziwa ya mtoto yaani upo LOOSE hata humpokei salamu yenyewe “MBONA UMECHELEWA KURUDI WE BABA NANII? " kisha maagizo kwa housegirl.
Mwanamke unatakiwa kutambua kuwa ubunifu na mbwembwe katika ndoa ili kumridhisha mmeo ndio nguzo kuu ya kumtuliza bila hivyo hata uombe maombi ya kujichanja damu bado atachepuka tu, maana nyumbani humjali, humpetpet, humfariji, hujisafishi, hunukii, humkarimu WAKATI mtaani kwa mchepuko anapetpetiwa, anaogeshwa, analishwa, ananyweshwa, anabembelezwa, anafarijiwa, anatiwa moyo, anaitwa majina mazuri BABY, HONEY, MY KING, MY SWEET POTATO, MY CHOCOLATE, MY EVERYTHING, MY RONALDO hahahahahaaaaaa hivi unafikiri kwa mchepuko huo atabanduka kweli??!!!!......
Maandiko matakatifu yanasema,
"Mwanamke mpumbavu ataivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe "
USIMPE MTU DHAMANA YA KUMHUDUMIA MMEO, UTAJA JUTIA BURE....
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/hivi-ndivyo-wanawake-wengi.html

No comments:

Post a Comment