Upendo ni kutoa kile kizima ulichonacho moyoni mwako kadiri ya uwezo wako ulionao kwa ajili ya kumpenda yule ulienae.
Upendo ni kwa ajili yako na mtu umpendae .. Yeye ni sababu ya wewe kumpenda .. Na wewe uwe sababu ya yeye kukupenda. Usiingie kwenye mahusiano ili upate kupendwa tu ..Bali ingia kwa ajili ya kwenda kupenda(kupendana).
Hata Biblia inatuambia alianza kutupenda ... Alituumba ili atupende ...nasi tukampenda ..lakini yeye alitupenda zaidi.. Hivyo anzisha mahusiano ili kupenda. Kupenda sio vibaya ..bali vibaya ni kutaka kupendwa angali wewe hujui maana ya kupenda.Yaani hurudishi kama anavyokupa.
Saikolojia ya upendo inasema kama hujui maana ya kupenda hata upendwe vipi hautaeshimu upendo unaopewa.
Kupendwa haufundishwi bali ni namna wewe unavyojitazama, ni namna wewe usivyopenda kutendewa mabaya, ni namna wewe unavyotaka kueshimiwa, ni namna wewe unavyotaka yule akupendae akujali .. Hivyo hivyo mtendee na mwenzako.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/muda-mwingine-tunatakiwa-kujua-upendo.html
No comments:
Post a Comment