Wednesday, February 12, 2020

HATA KAMA UMEUMIZWA SANA,BADO UNAYO NAFASI YA KUPENDA TENA.


Wapendwa baada ya kusikia malalamiko kutoka kwenu wadau wangu,wasomaji wangu kadhaa wengi wanalia kutokana na kuumizwa na wenzi wao ki­asi cha wengine kufikia hatua ya kujiapiza kwamba hawawezi tena kupenda.
''Aiseee sitowalaum na kwa hili no kuchekana''
Unapozungumzia suala la maumivu ya mapenzi, japokuwa huumiza sana hasa kama ulikuwa na mapenzi ya dhati na mwenzi wako na baadaye akaaamua kukugeuka,siyo suala geni hapa duniani.
Kama kwako ujakumbana nalo shukuru Mungu ila jiandae kiakili,ipo siku utakuja kuonja,ni changamoto kama ilivyo changamoto kwenye maisha.
Unapolia leo kwa sababu ya mapenzi, elewa kwamba ma­milioni ya watu wa­nalia kama wewe ingawa tunato­fautiana namna ya kukabiliana na maumivu.
Lakini cha kujiuliza ni je, mpen­zi wako akikuumiza sana, ni sahihi kujiapi­za kwamba hutapen­da tena?
Ni sahihi kusema kwamba siku hizi hakuna mapenzi ya ukweli kwa sababu tu amekuumiza?
Ni sahihi kusema wanaume wote wako hivyohivyo au wanawake wote ndivyo walivyo?
Ukweli ni kwamba, unapovunjika moyo haimaanishi kwamba huo ndiyo mwisho wako wa kupenda.
Unapo­jiapiza kwamba hutapenda tena au hutamwamini mtu tena,ni makosa makubwa kwa sababu kama uliyekuwa naye ameshindwa kuiona thamani ya penzi lako, yupo ambaye atakuthamini na kukuheshimu atakujali.
Kuna usemi maarufu kwamba mlango mmoja unapojifunga, mwingine huwa unafunguka muda huohuo lakini wengi wetu hupoteza muda mrefu kuutazama ule uliojifunga badala ya kuufuata ule ul­iofunguka some time tunaganda Bandarini kungoja ndege itue ili hali tunaelewa haiwezekani.
Msemo huo una maana kubwa kwenye mapenzi kwamba kama mwenzi wako amekutenda,amekuvunja moyo, amekusononesha na kukufanya ulie,jua kwamba hakuwa riziki yako.
Huwezi kujua Mungu amekuepusha na nini kwa hiyo badala ya kujiapiza na kumkufuru Mungu,ni bora ukakubaliana na ukweli,japo huwa inauma sana.
Ukishaukubali ukweli,unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupona maje­raha ndani ya moyo wako na nakuhak­ikishia,hata kama ulimpenda vipi huyo uliyekuwa naye,kama amefikia hatua ya kukuumiza na kuuvunja moyo wako, tabua hakua riziki yako, riziki yako yaja hebu acha AENDE.
Image may contain: 1 person


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/hata-kama-umeumizwa-sanabado-unayo.html

No comments:

Post a Comment