Wednesday, February 5, 2020

Mtu ukipenda yakupasa uangalie kwa kupenda sio kila mtu wa kupendwa

"Mtu ukipenda yakupasa uangalie kwa kupenda sio kila mtu wa kupendwa kisa hichi kimemkuta dada yetu Jackline alikuwa anapenda kwa moyo wake wote lakini anaishia kupata maumivu makali na kuufanya moyo wake kuraruka na kujiona kama ana mkosi alijaliwa kila kitu alipata kazi nzuri na nyumba nzuri lakini alikuwa kakosa kitu kimoja tu ndicho kilichomfanya aanze kukitafuta na si kingine ni mwanaume wa kumfariji pindi achokapo,
Wanaume wengi walimpenda Jackline kwaajili ya mali zake awakuwa na mapenzi ya dhati kwake yeye lile tukio lilimfanya Jackline asiwe na mwanaume mmoja alikuwa anajaribu kila mahali akishindwa huku anakwenda huku katika pilikapilika zake alikutana na wanaume kama watano ambao wenye tabia tofauti tofauti wapo waliomsaliti pia wapo wale waliokuwa na tamaa za mali zake katika maumivu aliyopitia yote lakini akukata tamaa ya kupenda ndipo akaja kukutana na mwanaume mwengine akijua huyo ndiyo pumzisho langu kumbe naye huyo ni pasua kichwa mwanaume huyo alitambulika kwa jina la John Jackline aliishi na John takribani mwezi mmoja akujua matendo ya John hata siku moja ndipo siku akaja kugundua kwamba John akutulia kabisa na mwanamke mmoja yeye alikuwa ni mtu wa kubadilisha kila nguo inayompendeza na maanisha kila mwanamke anayempendeza wanawake wengine alikuwa anaingia nao hadi chumbani kwa Jackline bila shaka,
Siku moja wakati John akiwa na mwanamke mwengine katika chumba cha Jackline bila kujua kama Jackline siku hiyo akwenda kazini alishinda nyumbani wakiwa chumbani wakipiga soga zile sauti zilimshtua Jackline kwa wakati ule alikuwa jikoni anasafisha baadhi ya vyombo ikabidi afuatilie hao watu wanaongelea wapi akajakugundua walikuwa wanaongelea chumbani kwake basi ikabidi atoke aende upande wa dirishani kwa bahati nzuri dirisha lilikuwa wazi kwahiyo akaona kila kitu kilichokuwa kinaendelea ndani,
Alimuona John akiwa na mwanamke mwengine wakiwa kwenye kitanda chake tukio lile lilimuuma sana lakini alijikaza na kutofanya vurugu akahamua kuchukua gari lake na kwenda bar kupoteza mawazo huku akimuacha John akistarehe na mwanamke asiyemjua John tabia yake ile aliendelea nayo akijua Jackline bado ajashtukia mchezo wake anaoufanya kumbe Jackline tokea siku ile alivyofumania alikuwa anamfuatilia nyendo zote anazofanya bila yeye mwenyewe kujijua,
Jackline moyo wake ulikuwa na maumivu ya ndani kwa ndani kutokana kuumizwa sana na John hali ile ilimfanya adhoofike na kazini asifanye kazi zake kwa ufanisi mawazo yalimtawala mpaka ikapelekea kuongea mwenyewe kila mahali kama chizi Jackline uvumilivu wake ulimponza akijua John atakuja badilika kumbe ndiyo kwanza anazidisha ufuska basi maumivu yale aliyokuwa anayapata yakamsababishia akili zake kupungua na kuwa chizi mazima akawa anatukana na kuwapiga watu ambao anaokutana nao kila sehemu huku akimuacha John akitumia mali zake bila wasiwasi na kuendelea kufanya starehe na wanawake wengine."
KUPENDA UGONJWA WA MOYO KATU SITOSAHAU MAUMIVU YA NDANI KWA NDANI...


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mtu-ukipenda-yakupasa-uangalie-kwa.html

No comments:

Post a Comment