Sunday, February 9, 2020

πŸ‡KWENU WANANDOAπŸ‡

Image may contain: 1 person, outdoor

Kila mmoja kati yetu anahitaji amani upendo na utulivu Wa nafsi yake katika maisha yake yote.πŸ‡

Ewe Dada,nyumba yako inahitaji kua sehemu tulivu kwa ajili yako na familia yako,eneo ambalo watapata amani na upendo kuliko pengine popote.πŸ‡

Wewe kama Mke ndani ya nyumba unatakiwa kua nguzo muhimu ya kujenga amani hio.πŸ‡

Maisha yote ya mwanamme ni mapambano ya kutafuta maisha, anaporudi nyumbani anahitaji sehemu tulivu kuweza kupata nguvu mpya baada ya mahangaiko ya mchana kutwa.πŸ‡

Yeye kua na amani sio muhimu kwake tu, bali kwenu nyote, epuka maneno na lawama zisizo na tija, epuka kununa nuna ovyo, epuka kumdhania mumeo vibaya, wivu ni sunna ila usipitilize mpaka ikawa karaha kwa mwenzako.πŸ‡

Enyi wanandoa ambao hamna bashasha mkiwa na pamoja, kumbukeni kua maisha ya dunia ni mafupi sana furahieni neema za Mungu ,ndoa na upendo ni starehe kubwa ambayo Allah ametujaalia kwanini muifanye nyumba yenu kama uwanja Wa mapambano na vita?πŸ‡

Kuna wanaume wakiingia majumbani Mke na watoto wanajikunja starring ameingia,mwanamke anakua hayuko huru ,hata akiwa na kitu anataka aongee na mumewe anajishauri anakaripiwa kama mtoto.πŸ‡

Acha kumkaripia Mke wako ovyo tena hadharani ,maneno yanauma kuliko bakora .Anapokosea mueleweshe kistaarabu atakuelewa zaidi.πŸ‡

Simaanishi kua hamtozozana ,lakini ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu kutengeneza mazingira ya amani na upendo na kuepuka mikwaruzano ya mara kwa mara.πŸ‡

*πŸ‡Nyumba yenye amani na upendo ,Mungu anazidisha neema na baraka na maendeleo.πŸ‡*
πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡πŸ‡


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwenu-wanandoa.html

No comments:

Post a Comment