Sunday, February 9, 2020

πŸ’ž *LEO NAWASHAURI WANAUME* πŸ’ž


Image may contain: 1 person, standing, text that says "BOSCH"

➡️ *EWE MWANAUME.......*

1). Mwanamke si ruler iliyonyooka kwamba hakosei, bali anapokosea adhabu yake si ngumi bali ni mawaidha πŸ’ž

2). Usihuzunike mkeo hapendezi au hanukii hali ya kuwa hujanunua nguo wala perfume ,wewe ndiye ulaumiwe πŸ’ž

3). Usifichue udhaifu wa mkeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mkeo, naye ni mlinzi wako πŸ’ž

4). Usimkataze mkeo kushika simu yako baada ya kuita kwa kuiwahi wewe kabla hajaona anayekupigia, unachokichukulia tahadhari kikigundulika ndoa yenu itapata mitikisiko πŸ’ž

5). Usiogope kuchekwa kwa kumsaidia mkeo shughuli za ndani, mke si mtumwa isipokuwa ni msaada kwako πŸ’ž

6). Usipendepende kusifu wanawake wengine mbele yake, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka πŸ’ž

7). Usimgombeshe mkeo kwa kutoweza kupika vyakula unavyovipenda ,kwao hakukua na chuo cha upishi alipika kulingana na kinachopatikana, bora ni kumfundisha πŸ’ž

8). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mkeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mkeo ni jukumu lako mwenyewe πŸ’ž

9). Hakuna mwanamke ambaye atamvumilia mwanaume dhaifu kitandani ,tumia kiwiliwili chako vizuri πŸ’ž

10). Peracetamol na dicloper isiwe ndio tiba ya kila ugonjwa anaoumwa mkeo ,suala la kumtibu ni lako usilikwepe πŸ’ž

11). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mkeo πŸ’ž

12). Usimlinganishe mkeo na wanawake wa nje hao hawajui thamani yako ,ukiendelea na hilo mapenzi ndani yatapungua πŸ’ž

13). Muheshimu mkeo hata kama wewe ndio mkuu wa familia kwani heshima ndio msingi wa ndoa yenu πŸ’ž

14). Usiwe mume mwenye dhana potovu juu ya mke ,uwaminifu ndidi ya mkeo ndiyo chanda njema πŸ’ž

15). Usimkosoe mkeo hadharani anapokosea ,hakuna anayekubali kukosolewa hadharani ,matoke ya hilo siku zote huwa hasi πŸ’ž

17). Maamkizi mema yapambanishwe na kugusana miili yenu ,jambo hilo huondoa madoa yaliyo katika nafsi zenu πŸ’ž

18). Neno "nakupenda" litawale kumwambia mkeo kwani mwanamke hufurahi kuambiwa neno hilo πŸ’ž

19). Penda kumshirikisha mkeo katika mipango ya kimaendeleo, mwanamke ni mshauri mzuri πŸ’ž

20). Watoto ni watoaji nje kila habari iliyo ndani kwenu, hivyo sehemu ya kumkosoa ni chumbami si mbele ya watoto πŸ’ž

21). Usimlaumu mkeo kwa kumkuta akiwa hayuko katika hali ya usafi, sms pia ingetosha kumjulisha kwamba unakuja ili ajiandae πŸ’ž

22). Wazazi unatakiwa kuwafanyia wema lakini usijisahau kiasi cha kusahau wajibu wako kwa mkeo ,uadilifu wako ndio utakaofanya wawili hawa waishi kwa upendo πŸ’ž

23). Usisahau kuwa mke anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye usiwe kama kamanda wa polisi, Mawasiliano yenye utulivu ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha πŸ’ž

24). Iwapo mawazo yeke hayakufanikisha jambo kuliko mawazo yako, usimpuuze Bali ishini na mfanye kazi kama timu πŸ’ž

25). Maskani na vibaraza sio katika misingi ya ndoa ,kaa na mkeo ,mwanamke hupenda kumuona mwenza wake mara kwa mara πŸ’ž

26). Mfanyie suprise mkeo hata kwa chokolate ,hilo litaamsha hisia zake na kujiona unamjali πŸ’ž

27). Usisuhubiane na wanaume wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa, kwani wavurugaji wa ndoa za watu ni binadamu wa kawaida,ulinzi wa ndoa yako ni jukumu lako πŸ’ž

28). Kumuoa wewe mkeo sikuvunja udugu wao panapo haja mpe ruhusa akawasamilie ndugu zake πŸ’ž

29). Umri au kuoa mke mwingine isiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa πŸ’ž

30). Wewe ndiye utakwenda kuulizwa mbele ya Mola muumba ,usimamizi wa ibada katika familia ni jumu lako πŸ’ž

πŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’žπŸ’ž


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/leo-nawashauri-wanaume.html

No comments:

Post a Comment