Friday, February 7, 2020

Kuna jambo kila mtu anatakiwa kuliamua kwa sababu ya amani na furaha ya maisha yake.

%"FURAHA YAKO"%

Kama upo katika mahusiano ya amani na furaha, unatakiwa kuamua kuwa bora zaidi ili amani na furaha yako iweze kuendelea.
Ni vigumu sana kuendelea kufurahishwa na mwenzako ikiwa unafanya matendo ya kuudhi na kuumiza.
Kama unataka kuona amani na furaha uliyonayo katika mahusiano yako inadumu basi kuwa mtu bora na sahii katika maisha yake.
Kwa kila kitendo unachotakiwa kufanya hakikisha unakifanya kwa namna inayotakiwa, ila kaa mbali na epuka kufanya yale yasiyo mpendeza mwenza wako ili kumfanya awe na amani na utulivu wa nafsi nyakati zote.
Kwa maendeleo ya furaha yako amua kumpa amani na furaha.
"Katika mahusiano furaha huwa ni kitu kinachosababishwa na kutengenezwa pamoja hasa mkiwa mnapendana.
Kama unataka furaha na amani inabidi umsababishe yeye kuwa na amani na furaha.
"kama ukimfanyia ujinga leo, kuna hatari hata yeye naye kukufanyia ujinga kesho".
By,
J4REAL-TECK


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kuna-jambo-kila-mtu-anatakiwa-kuliamua.html

No comments:

Post a Comment