Friday, February 7, 2020

Mwanaume hujaribiwa na Shetani akiwa na hela. Lakini

Mwanaume hujaribiwa na Shetani akiwa na hela. Lakini shetani
humkimbia akiishiwa.
Angalia wanaume wengi wakiwa na hela wanavyo behave. Hawajali familia zao, attention yao kubwa ni kwenye ulevi, vimada, disco, kamari, makasino etc.
Lakini wakiishiwa wanashinda nyumbani, wanajali familia, wanapanga mipango ya maendeleo (ambayo mingi haitekelezeki
akishapata hela).
Na Mwanamke hujaribiwa na Shetani
akiwa ameishiwa, na shetani humkimbia akipata hela.
Angalia wanawake wengi wakiwa na hela
wanavyojiamini, hawajirahisi hovyo kwa wanaume, wanapanga
maendeleo ya familia zao.
Lakini mwanamke akiishiwa anakuwa hopeless.
Anapoteza matumaini, ni rahisi kuanguka dhambini ili apate pesa.
Uzinzi, ulevi etc.
Yuko tayari kutoa
mwili wake ili apate fedha za kuikimu familia yake.
Nini kifanyike? Mwanaume ukipata pesa usikae nazo, mpe mkeo azitunze halafu mzipangie matumizi zikiwa kwake.
Ili shetani akija kukujaribu akute umeishiwa, na akienda kumjaribu mkeo amkute amejaa mahela.
Ni ngumu ila ina wezekana.
AHSANTENI.
J4REAL-TECK


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanaume-hujaribiwa-na-shetani-akiwa-na.html

No comments:

Post a Comment