Monday, February 10, 2020

KAMA KWELI UNAMPENDA....FANYA HILI


Sogeza ndimi yako kando ya sikio lake,kisha mpenyezee sauti nyembamba uliyobeba joto la kinywa chako
Walau umwambie,
Mpenzi! Niliutambua uhodari wako ndiyo maana sikutaka ushauri kukukabidhi moyo wangu. Wewe ndiye mwanamke ambaye mara kwa mara niliwaza kusafari naye jahazi moja la mapenzi. Ahsante kwa kuyafanya mawazo yangu kuwa kweli.
Ahsante sana!
Mpenzi! Endelea kulea hisia zangu kwa moyo wa kujitolea,usihitaji malipo ukanikumbusha ya nyuma.
Ishi nami kwa dhana ya hakuna mafanikio ya mwanaume isipokuwa nyuma kuna mwanamke. Nami nitaishi nawe kwa dhana ya mwanamke kutokea ubavuni mwa mwanaume.
Mpenzi! Najivunia uwepo wako.
Najivunia mno.
Umekuwa mwanamke wa kwanza kuziongoza hisia zangu mahala nilipotamani zifike.
Hujawahi zipeleka kando ingawa si zako,nadhani umezichanganya na zako ndiyo maana sijawahi jutia kuwa nawe.
Sina budi kujivunia.
Nawe nataka ujivunie uwepo wangu kwa kukufanya usijute.
Usijute kuwa nami,bali ujute kwa nini hukuwa nami mapema.
Nitahakikisha nakuwa mpishi wa moyo wako kwa kukupaka harufu ya maneno mazuri.
Penda sana kudeka kwa makusudi,nami nakuahidi kukudekeza kila udekapo.
Unionapo nalia baada ya kukutazama,usihuzunike ukadhani umenikosea. Nalia kwa furaha,mapenzi unayonipa sijawahi yagumia.
Nahisi kama ulitumwa uje kuniuguza mhanga mimi wa mapenzi niliyechakazwa na wenye mapenzi ya riba. Mapenzi ya nipe pesa nikupe mwili kama huna kafie mbele.
Nasema ahsante kwa hilo!
Mpenzi,moyo wangu na wako kwa mapenzi yet ndiyo sababu ya kuwa pamoja. Nakusihi kaa mbali na mengine uyasikiayo kwa ndugu,jamaa,marafiki ama majerani.
Kumbuka chema hakikosi kusakamwa hasa kwa wenye chuki.
Ikibidi niulize,isipobidi mezea ili wambea waulizane.
Mpenzi,moyo wangu umebeba mengi nipasayo kukueleza.
Mengi mno!
Lakini tosheka na haya machache ingawa hayajakidhi kiu yako.
Usijali,nishakupa mwanya wa kudeka hivyo kesho nayo ni siku.
Nidekee ili nikupenyezee mengine ujivunie uwepo wangu ubavuni pako.
Mungu amenipa elimu ya kutambua chakula cha hisia za mwanamke.
Nitazishibisha hisia zako kwa maneno mazuri usowahi pewa kabla.
Wewe ni sehemu ya mwili wangu,nisipokutunza nimejitupa mwenyewe.
Nakupenda unanipenda! Nitaendelea kukupenda.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kama-kweli-unampendafanya-hili_10.html

No comments:

Post a Comment