Monday, February 10, 2020

TOFAUTI YA HISIA NA AKILI KATIKA MAAMUZI KWENYE MAHUSIANO.


Hisia na akili huwa vinamaamuzi tofauti muda mwingi ..na hii inategemea kipi kitakuwa na nguvu kubwa ndani yako kuliko kingine.
Mfano:
Umempigia simu mpenzi wako mara ya kwanza hakupokea, mara pili akupokea mpaka mara tatu hakuweza kupokea simu yako ..baada ya masaa mawili akakupigia .. Maaongezi yatakayotoka kwako yatategemea kipi kina nguvu kuliko mwenzake, ni hisia au akili.
HISIA INAPOKUWA NA NGUVU KULIKO AKILI:
Maongezi yako yatakuwa hivi:
"Mbona napiga simu mara nyingi haupokei, ni dharau ama nini, naona hakuna umuhimu wa kukupigia simu yangu, kama umechoka kupigiwa simu uwe unasema." Hayo ni baadhi ya maneno..
Kumbuka kuwa mtu huyu huongea hivi kwa hisia ...anayo akili ya kupambanua lakini hisia imekamata akili yake ..kwa maneno mengine hisia ina-control akili yake.. Hivyo hafikiri tena kwa akili bali hufikiria kwa hisia.. Na hisia inapozidi haitaki kujua ukweli ni upi wala uongo ni upi kwa namna moja ama nyingine haitaki kujua ukweli bali jambo kama ili linapofika hisia ukimbilia kwenye part ya kuhisi unaonewa, unadharauliwa, unachezewa.
AKILI INAPOKUWA NA NGUVU KULIKO HISIA:
Kama ni mara ya kwanza anafanya jambo hili akili itataka kutafuta sababu ya kwanini amefanya hivi ...haitakurupuka na maneno ya moja kwa moja.
Mfano: akili inaweza kuhisi mtu huyu yuko mbali na simu hivyo hasikii ikiita ..na kama ni kawaida yake kufanya hivi, akili itakupa kazi kuitazama hii tabia kiundani ..kama ukija kugundua sio mtu wa kukaa na simu karibu basi haitakusumbua sana, kama utakuja kugundua akiwa na kazi nyingi sio mtu wa kupokea simu na hii imekuwa ni tabia yake pia haitakupeleka katika hisia mbovu.
Tambua kuwa akili huwa inagundua hapa ni dharau au kuna sababu ya simu kutopokelewa lakini hisia ukupelekea kuhisi jambo baya kwa mtu huyu moja kwa moja bila kutafuta sababu
Akili utafuta sababu ..haikurupuki kuhukumu..
Akili ukupa wazo la kutaka kujua kwa kuuliza na sio kulaumu ..ikisha fahamu ndio hutoa jibu lake.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/tofauti-ya-hisia-na-akili-katika.html

No comments:

Post a Comment