Monday, February 10, 2020

Suala la wadada kubeba mimba siku hizi limekua kama kitu cha kawaida ndiyo nawalaumu wadada kwakua pamoja na kuona namna wenzao wanavyoteseka,

Suala la wadada kubeba mimba siku hizi limekua kama kitu cha kawaida ndiyo nawalaumu wadada kwakua pamoja na kuona namna wenzao wanavyoteseka,  pamoja na kuona kua hata katika mahusiano yao wanapitia magumu lakini bado wanaendelea katika kuingia kwenye mtego. Mtu uliyemfumania juzi bado unaennda kufanya mapenzi naye kavukavu siku za hatari halafu unategemea alee mtoto.
Nadhani ungejifunza hata kalenda yako kwanza kabla ya kuanza mapenzi. Lakini tuachane na hilo, si mada yangu leo, mada yangu na kitu ambacho naona kimekua cha kila siku ni hili suala la mwanamke unabeba mimba halafu ukishamuambia jaamaa tu nina mimba yako unataka akajitambulishe kwenu, alete Barua au atoe hata Mahari, wengine hutaka Ndoa kabisa!
Dada yangu mtu hajakuambia kuwa naataka kukuoa unataka ajitambulishe kwenu ili nini? Inawezekana hata mpango wa Ndoa alikua hana au hata kama alikua nao ana mchumba wake, tena inawezekana hata unamjua huyo mchumba wake lakini bado ulikua unang’ang’nia au ana mtu mwingine na ulijua au ukabeba na mimba kabisa sasa unataka ajitambulishe.
Wanaume siku hizi ni wajanja, anajua akishajitambulisha, akija kwenu hata kama ni kuseme mimba ni yangu ndiyo kashaoa. Niseme tu wazi mtu kukupa mimba si kigezo cha kukuoa, nataka muelewe ili mkibeba mimba mjue kua mimba sio tiketi ya ndoa. Kama unabeba mimba ukidhani umepanda basi la ndoa basi unajidanganya, si kwa karine hii.
Unapokubali kubeba mimba ya mwanaume, awe amesema nitakudumia, awe kajitambulisha kwenu na hata kutoa mahari kama hajakuoa, kama hamjafunga Ndoa Kanisani, Msikitini au kwa Mkuu wa wilaya basi wewe ni umepanda basi la ‘Single Mother’ ndiyo ukweli huo, muwe mnaupenda hamuupendi ila kama utabeba mimba ya mtu ukitegemea atakuoa basi utasubiri sana, atakuoa kwakua anakupenda na si kwakua umebeba mimba yake..
makengo


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/suala-la-wadada-kubeba-mimba-siku-hizi.html

No comments:

Post a Comment