Tuesday, February 11, 2020

Jifunze Lugha Za Mapenzi lasivyo utaishia kuachwa na warembo kila siku


Hakuna linalouma moyo kama mtu kuachana na aliyempenda. Moyo husafiri kilometa nyingi kwa kuwaza. Hakukosea aliyesema sikitiko la mahaba linashinda msiba. Lakini yote hayo yanaweza kuepukika na kukaa mstari ulionyooka endapo mawasiliano yatabeba umuhimu unaotosheleza na kusimama kwenye nguzo zake kuu.
MAWASILIANO: Ni nguzo kuu ya uhusiano. Ikiimarishwa huchochea amani ya kudumu lakini kinyume chake ni kichocheo cha wapenzi kuachana. Ni vizuri kujifunza lugha inayoweza kukufanya uelewane na mwenzako. Sauti yako ukiwa mtaani itofautiane na ile ambayo unaitumia chumbani.
Pengine una kawaida ya kutoa majibu ya mkato unapokuwa unazungumza na rafiki zako, lakini tabia hiyo hutakiwi kuizoea pale unapokuwa na mwenzio chumbani. Ikiwa umezoea kuwaita wenzako: “Wewe!” Mwenzi wako hutakiwi kumwita hivyo.
Ni elimu ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwamba kutofautisha maeneo ni jambo la busara. Kwamba sura yako iwe nyingine unapokutana na watu wa mitaani, itofautiane unapokuwa na wazazi, vivyo hivyo pale ambapo upo sehemu ‘spesho’ na mwenzi wako.
Lazima uwe unabadilika kama kinyonga. Ukiwa kazini mbele ya watu unaowaongoza unazungumza kwa sauti ya amri, lakini hiyo hupaswi kuitumia unapokuwa na wazazi wako. Unaongea kwa sauti kali ya kuamrisha mbele ya baba yako, hiyo adabu umefundishwa wapi?
Kuna lugha ya kuzungumza ukiwa na mwenzi wako. Ni mwiko kutoa sauti ya kuamrisha. Ni vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho kitakufanya uonekane una kasoro za kisaikolojia. Tawile kwa kila linalosemwa na mpenzi wako hairuhusiwi, unatakiwa kuweka mbele hisia zako.
Upole kupitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi. Eti, utaonekana una nidhamu na unamsikiliza vizuri mwenzio, la hasha! Utatambulika kuwa mtu hai kulingana na jinsi akili yako inavyofanya kazi.
.....inaendelea like page


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/jifunze-lugha-za-mapenzi-lasivyo.html

No comments:

Post a Comment