Thursday, February 13, 2020

SIRI KUBWA KUHUSU MWANAMUME


Mungu alimuumba Mwanadamu Kwa Sura na Kwa mfano wake na alimuumba MWANAMME na MWANAMKE Mungu aliwaumba ukisoma mwanzo vzuri utagundua wote waliumbwa Siku moja katika Roho Ila udhihirisho Mwanaume alitangulia Kuumbwa Ndipo akafuata mwanamke Ambaye n ubavu wake
Mwanzo 1:27
Asili ya Mwanaume ni Mungu lakini Asili ya mwanamke ni mwanaume tamanio la Mwanaume ni Mungu lakini tamanio la mwanamke ni Mwanaume Hivyo Mwanaume Ni Mungu Kwa Mwanamke
Siku moja Paulo akiwa Korinto akawa akiwafundisha makutano na kuwaonyesha Baadhi ya mambo ukisoma 1Wakorinto 11:7-9
Note nanukuu....
Kwa maana kwel haimpasi mwanamume kufunika kichwa kwasababu yeye n mfano na Utukufu wa Mungu ,Lakini mwanamke ni Utukufu wa mwanamume
8:-Maana mwanamume hakutoka Katika mwanamke Bali mwanamke katika mwanamume
9:-Wala mwanaume hakuumbwa Kwaajil ya mwanamke ,Bali mwanamke Kwaajil ya Mwanaume
10:-Kwahiyo imempasa mwanamke awe na dalili yakumilikiwa kichwani Kwaajil ya malaika
Baraka za Wanawake wengi ziko kwenye Mikono ya wanaume ,heshima ya wanawake wengi iko kwenye Mikono ya wanaume Na ndio maana Mwanamke anapoolewa Anapata heshima Kubwa na kuonekana kuwa wathamani baada yakuwa amemilikiwa Maana Yeye hawezi kumuona Mungu pasipo Mwanaume (Kiroho)
Kwanini Yesu alikuja Kwa Picha ya Mwanaume na sio mwanamke ????
Ufalme Uko kwenye Mikono Ya mwanaume Hakuna Ufalme ambao uko kwenye Mikono ya mwanamke ndio maana Mungu alivyotaka kuja kuutambulisha Ufalme Duniani alikuja Kwa Picha ya Mwanaume Maana Ufalme uko katika Mwanaume ...
Kichwa cha Familia ni Mwanaume
Kichwa cha Kanisa ni Kristo
Mwili wa familia ni mwanamke
Kanisa lenyewe ni mwanamke
Maongozi ya familia Yako katika Mwanaume Maana Ndiye dereva au kiongozi wa familia na Mungu akitaka kufanya Jambo kwenye familia anaanza kuongea na Huyo ambaye n kichwa inategemea kuwa amekaaje na Mungu Ila hiyo n nafasi yake yeye kupata maongozi ya KIUNGU Kwa familia yake
Mwanaume n Alama Kubwa inayomtambulsha Mungu hapa duniani
N Ufalme mkubwa ambao uko kwenye himaya ya Mungu hapa duniani
Mwanaume anasehemu Kubwa hapa duniani kumbuka hata Jina la mwanamke lilitoka kwenye kinywa cha mwanaume Adamu alimuita Hawa hivyo Hakuna utambulisho wowote hapa duniani Kwa mwanamke bila kuwa na mwanaume ..
Leo hii Dunia inasahau Sheria za Mungu
Wanawake wengi wako Tyr kukaa juu ya Waume zao waamue kwao Wakae kama Baba kwenye familia na kuamini kuwa Yeye Ndiye ambaye anapaswa kuwa na nafasi kuliko mwanaume
Acha nikuambie Mpendwa anaweza kuwa mwanaume Haongei wala Hana neno Ananyenyekea na wewe unajivunia kuwa umemuweka kwenye Mikono yako na kujisifia Kwa wenzako lakini wewe mwenyewe Umefunga milango yako Ya baraka na Neema Kubwa Kwa nyumba yako
Ndio maana ukisoma biblia anasema kuwa mwanamke mpumbavu ataivunja Nyumba yake Kwa Mikono take mwenyewe Usisahau kuwa Pia anaweza kuijenga Kwa Mikono yake mwenyewe kama akiwa mwerevu
Kwanini leo tumekuwa na wimbi Kubwa la Laana na umasikini kwenye maisha yetu na Hata unahisi n Mungu ametuacha ni kwasababu Nafasi za Ufalme zinataka kukaliwa na Wanawake na wakati hizo n za wanaume
Chanzo cha mambo Mengi
Chanzo cha Nyumba ndogo
Chanzo cha ukahaba na umalaya kupata nafasi huku duniani kinatokana na kuchukuliwa Kwa nafasi ya Mwanaume ndani ya Nyumba yake ...
Hesabu ya Mungu Huwaga iliangalia mbali Sana kusema Baba n kichwa
Na anapaswa kukupenda mke wake Lakini wewe mke wake umtii katika mambo Yote
Somo lijalo nitaongea Siri Kubwa Iliyoko Kwa mwanamke
Niambie nn umejifunza kwenye comment yako
Japo najua wanawake wengi hawata Comment (Watajifanya hawajaona) penda kujifunza ukwl uishi salama


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/siri-kubwa-kuhusu-mwanamume.html

No comments:

Post a Comment