Monday, February 3, 2020

MWANAMKE Ukiwa na Tabia Hizi 7, Lazima Mwanaume Akukimbie Hata kama unajijua Kuwa ni mzuri kupita uwajuao kuwa unawazidi kiwango, utaishia kuachika na kuona wasio wazuri wakiolewa.


Image may contain: 4 people
Mtia Moyo
1. CHOKOCHOKO
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. KUTORIDHIKA
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.

Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. KULINGANISHA
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’

Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. KUWA TEGEMEZI
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.

Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. KUTOKUA MUELEWA
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.

Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. KUJITAPA KWA KUWA NACHO
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. KUWA BIZE SANA
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize.

Wakati ujao nakuja na tabia za wanaume zisizofaa, ili nao wajijue na wawe na tahadhari wawapo na wake zao na si kujiachia wakajisahau.

Njia NANE zitakazokuonesha kwamba MWANAMKE uliye naye atakusaidia kuleta mafanikio katika Ndoa yako!

Katika moja ya Interview ambayo Barack Obama alifanya na jarida la "Black Enterprise Magazine" la nchini Marekani, muandishi alimuuliza kuhusiana na hali ya uchumi ya Marekani.

Aliulizwa, "Bwana Obama, Je una hofu juu ya hali ya uchumi wa Marekani inavyoenda?"

Ambapo Obama alijibu, "Hapana, sihofii uchumi wa Marekani, nina hofu na mke wangu..kwa sababu ana idea nyingi kichwani mwake mpaka nashangaa"

Hivyo, kama unae mwanamke anaekutia moyo ufanye vizuri zaidi. Huyo mwanamke ni keeper, kama hujamuoa, basi anastahili pete kidoleni kwake

Hapa chini nimeelezea njia NANE zitakazokuonesha kwamba Girlfriend wako anafaa kuwa mke kukusaidia ndoto za mafanikio na ndoa imara!

1. Anavaa kimafanikio (she dresses for Success, not to Seduce)

Kama kitu ambacho kinawatofautisha wanawake wenye mafanikio na wengine ni mavazi wanayovaa. Wanawake wasio na focus huvaa mavazi ya kushawishi, lakini wanawake walio focused huvaa nguo za heshima. Wanawake wote wenye mafanikio kwa jitihada zao halali huvaa kiheshima, kuanzia Marissa Mayer, Oprah Winfrey au Michelle Obama. Kile unachovaa, kinaeleza kwa undani namna tabia na mwenendo wako ulivyo!

2. Huishi kulingana na kipato alichonacho.

Hii haimaanishi anaishi kimasikini. Hapana, inamaanisha anampangilio mzuri wa fedha anazozipata kwa halali yake. Kwamba katika fedha yake, anayapa kipaumbele mambo ya msingi, kwamba yuko tayari aishi kwa kujibana sasa hivi ili baadae aishi kama Malikia.

3. Hana marafiki wengi na amezungukwa na marafiki ambao ni problem solvers na sio attention seekers.

Hebu nioneshe mwanamke yeyote mwenye mafanikio, na mimi nitakuonesha mwanamke mwenye mtandao wa marafiki ambao ni World changers wale wanawake wanaopenda mafanikio.

Kama Zig Ziglar alivyowahi kusema kwenye kitabu chake cha "Over the Top", "Zungukwa na watu ambao watakutia moyo na watakupa hasira ya kuinuka juu ya pale ulipo"

Hivyo, utatambua mwanamke wako atakuja kuwa vipi kwa kuangalia marafiki anaochangamana nao.

4. Huilaumu nafsi yake, sio jinsia yake.

Tofauti na wanawake wengine, mwanamke mwenye kiu ya mafanikio hapotezi muda kulalamika kuhusu vikwazo anavyopata kwenye biashara au kazini kutokana na jinsia yake pale anapofeli jambo. Badala yake, hukabiliana na changamoto za yeye kuwa mwanamke kazini, na kuzitafutia ufumbuzi. Hautakuja kusikia mwanamke mwenye mafanikio analalamika kufeli jambo kisa yeye ni mwanamke.

5. Huwa na imani ya mafanikio.

Namaanisha, hujiamini na huiamini nafsi yake kuwa anao uwezo wa kufanikiwa. Kama founder wa magari aina ya Ford Ranger, Henry Ford katika kitabu chake cha "My life and Work" alivyosema kuwa, "Uko sahihi vyovyote vile utakavyofikiria, kama utafikiria unaweza uko sahihi, na kama utafikiria hauwezi uko sahihi vilevile"

6. Huwasaidia wanawake wenzake.

Moja ya jambo ambalo nimejifunza katika maisha yangu ni kwamba, tofauti na wanaume ambao ni rahisi mno kuinuana na kusaidiana kwenye matatizo, wanawake hawapendani, na baadhi hufurahi wanapoona wenzao hawafanikiwi kuzidi wao.

Mwanamke wa kwanza kabisa kuwa secretary state wa Marekani Madeleine Albright amewahi kusema, "Kuna sehemu yao mbaya sana kwa wale wanawake ambao hawataki kusaidia, hawawapendi na wana wivu juu ya wanawake wenzao"

Mwanamke wako atafanikiwa, endapo atawapenda wanawake wenzake na kuwasaidia na wao wafanikiwe.

7. Yupo current, yuko updated na anafahamu mambo mbalimbali yanavyoenda.

Hii inamaanisha anajitahidi kuji-expose na maarifa mapya, taarifa, na idea mbalimbali ambazo zitamuinua kiakili na kifikra. Funguo za mafanikio zipo katika maarifa mapya. Kama Brian Tracy alivyowahi kusema, "to earn more, one has to learn more"

8. Yuko radhi kubeba risks.

Hii inamaanisha haoni hasara kupoteza katika uwekezaji, sio kwenye biashara tu, hata kuwekeza moyo wake kwako. Hata kama ataona haufanikiwi kwa hivi sasa, atakuamini, kiasi ya kwamba atawekeza roho yake, akili yake na hisia zake kwako.

Ngoja nimalizie kwa Hekima hii, Uwekezaji ulio bora kwa mwanamke sio kujaza nguo kwenye kabati, uwekezaji mzuri ni kupata yule mwanaume bora ambae MUNGU amekuchagulia!!

Utafanikiwa tu!

Tukutane muda mwingine kuelezea upande wa wanaume.

Share


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanamke-ukiwa-na-tabia-hizi-7-lazima.html

No comments:

Post a Comment