Sunday, February 9, 2020

*KWENU WADADA*

Image result for mapenzi wakubwa

*🍇Mke na majukumu🍇*

🍇Mahitaji ya nyumba hata kama uweke ma house girl kumi bado uangalizi wako unahitajika kwa kiasi kikubwa sana.

🍇Pia unapomweka msaidizi nyumbani unatakiwa uwe mpole mchukulie kama mdogo au mtoto wako kulingana na umri wake.  Hakikisha anafanya kazi lakini anapata muda wa kupumzika, ale chakula mnachotumia hapo nyumbani sio mnapika chakula kizuri ye anaambiwa asonge ugali tena na mboga iliyobaki sio vizuri hata Allah mtukufu  hapendii

🍇Hakikisha chakula cha mumeo unapika mwenyewe kama una nafasi ya kufanya hivyo na hasa weekend tumia muda wako vizuri kukaa na mumeo ndani mzungumze mambo ya watoto, maisha na n,k

🍇Badilisha chakula mara kwa mara sio chakula inakuwa sheria mchana ugali usiku wali kila siku iendayo kwa Allah mtukufu hapana shost utakimbiwa.

🍇Sasa hebu niseme na wewe mke wa mtu ambaye hutaki upitwe  harusi, kitchen, pati,send-off, kigodoro, beseni, birthday party, universary na sherehe zote za mjini we za kwako.

🍇Mumeo hana raha nawe kila siku kuomba pesa ya sare na kumrundikia kadi za michango saa zingine hata mwenye shughuli hamjui, mmh mtaendelea kweli?

🍇Huna muda wa kuangalia hata familia yako dada wa kazi ndio anakuwa mama mwenye nyumba ajue usafi wa nyumba, afue nguo za nyumba nzima, apike chakula, ahudumie watoto, amhudumie mumeo bado ukirudi kosa kidogo tu utamfokea na kumtishia kumfukuza kazi.

 Tena inawezekana kuwa ni kabinti kadogo sana

🍇Mshahara mdogo na akivunja glass unamkata, jamani jiulize angekuwa mwanao jee ungefurahi?  Ndio maana wengine wanageuka nyumba ndogo

 Binty anaamshwa saa kumi na moja alfajiri na kulala saa tano usiku kila siku

🍇Hata watoto wetu wa sasa wanaharibika kwa kukosa uangalizi wa karibu hasa wa mama.

*🍇Fungua macho ewe dadangu🍇*


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwenu-wadada.html

No comments:

Post a Comment