Monday, February 10, 2020

KWA NINI TUNASHINDWA KUISHI KAMA MARAFIKI MPAKA WAKATI WA NDOA NDIPO TUSHIRIKI TENDO?:

 Imekuwa ni suala gumu kwa wachumba kufurahia urafiki wao kabla ya ndoa pasipo kufanya mapenzi. Wazungu wenzetu wamekuwa wakiishi kwa upendo na ukaribu pasipo hata kuogopana kwamba nikikaa na boyfriend ama mchumba wangu atatumia nguvu kunilazisha ngono tofauti na kwetu tunaoogopana kama simba na swala. Katika ulimwengu wa sasa vijana wanawaza ngono kama ishara ya kupendana kwao.Unakuta kijana hataki kuamini kama anapendwa kama binti atakataa kufanya naye mapenzi.Uaminifu na upendo wa binti unapimwa kwa kukubali kumvulia nguo rafiki ama mchumba wake. Jambo hili limefanya mabinti wengi kupoteza usichana wao(bikra) kabla ya ndoa.Yaani wenye hii kitu wameadimika kutokana na mabinti/vijana kukosa misimamo ya kuishi kama marafiki. Mbaya zaidi hata mabinti wenyewe wanaleta dharau badala ya kufurahia kumpata aliyetayari kumtunza hata kama ameshawahi kushiriki kabla hawajakutana. Honeymoon hakuvutii kwani hakuna haja ya shuka jeupe.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kwa-nini-tunashindwa-kuishi-kama.html

No comments:

Post a Comment