Monday, February 10, 2020

Dear Broher usije ukadhani Kumpa mimba mwanamke wako halafu ukamkimbia na kumfanya awe single mother itatuzuia sisi tunaojua thaman yake tusimpende πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜… pole sana

Dear Broher usije ukadhani Kumpa mimba mwanamke wako halafu ukamkimbia na kumfanya awe single mother itatuzuia sisi tunaojua thaman yake tusimpende πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜…πŸ˜… pole sana . Tutampenda, tutafunga nae ndoa, ataishi kwa furaha na atafurahia maisha mpaka ajutie muda aliokuwa akiupoteza kwako wewe hapo.
.
.
Kwa maana mwisho wa siku Single mother nae ni mwanamke kama wanawake wengine, anayo kila sababu ya kuhitaji kupendwa, kuolewa, na kuwa na mwanaume ampendae.
.
.

.
Yeye kuwa na mtoto hakumfanyi asivutie, asipendwe au aonekane disperate na kufanywa kama chombo cha starehe na wanaume wakware. Ndio, yeye ni mama na ni mwanamke pia, tena mwanamke mzuri ambaye ana a lot of things to offer!
Black bro, mpende kama wanawake wengine na usimuone kama yuko dillema ukatumia huo udhaifu wake. Usimuone kama anatafuta mwanaume wa kumsaidia kulea mtoto wake. Licha ya aliyopitia bado Hajavunjika moyo, she is not a mess!
.
.
Ni mwanamke mzuri, anayepambana na hali yake na wala hatafuti huruma. Anampenda mtoto wake kwa moyo wote, na anao upendo wa hali ya juu kwa mtu ambae ataonesha kumthamini. Mpende, na jaribu kuelewa mazingira yaliyomfanya mpaka akawa single mother, ukielewa hilo utajikuta ukimheshimu kwa yale aliyopitia!
.
.
Uhisi uzuri wake, muone namna anavyopenda it is beyond her motherhood, mtazame namna anavyomkuza mtoto wake, namna anavyomlea mwanae, inaonesha namna yeye binafsi alivyo. Ni rahisi mno kumpenda, ni rahisi mno kumpenda mtoto wake.
.
.
Single mother, ninyi ni wazuri. Mna moyo wa kulea; naamini siku moja mtakuja kuwa wake wazuri kwa mwanaume atakaetambua namna mlivyo!!
Aisee nawapenda single moms kuliko ilivyo kawaida kuzaa kwao haimaanishi wao walikuwa malaya NO NO NO NOOOOOOOOOOO!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/dear-broher-usije-ukadhani-kumpa-mimba.html

No comments:

Post a Comment