Monday, February 10, 2020

Kuna wakati mtu anayetaka kukuacha utamgundua kwa matendo yake anayokufanyia.

Anaweza asikwambie kwamba hakuhitaji ila atatoweka tuu kimya kimya.
Utaanza kuona tuu matendo yake sio ya upendo tena bali ni kama uadui. Kadiri siku zinavyosonga mawasiliano yanaanza kuwa hafifu au yatapotea kabisa hadi wewe utakapomtafuta ndio anaaza kujikosha kosha kwamba alikuwa amekumisi.
Mara nyengine anaweza akawa anakutuhumu katika kila jambo hata kama jambo hilo hujalifanya wewe, lengo ni kutafuta mazingira ya kukuacha. Anaweza akawa na kisirani cha mara kwa mara bila sababu za msingi na lawama za hapa na pale. Kwa ishara hizo chache unadhani sababu ya kumuuliza kwanini inakuwa hivyo?
Unaweza ukamuuliza na akakupa sababu za uwongo tuu kwamba bado anakuhitaji huku muda wako unaendelea kupotea. Kama hutotumia ishara hizo chache kujiongeza na kutafuta ustaarabu mwingine, utajikuta penzi limeshakufa umeachwa na maumivu makali moyoni mwako.
Chris JR


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/kuna-wakati-mtu-anayetaka-kukuacha.html

No comments:

Post a Comment