Usivunje uhusiano na mtu sababu tu umegundua kuwa sio rafiki.
Kwenye maisha hatuhitaji marafiki tu. Tunahitaji watu wote.
Kila mtu atakufaa kwa namna tofauti. Hata wale wasio marafiki, kuna kipindi watakufaa.
Sio kila mtu atakufaa kwenye biashara au kipindi unatafuta kazi.
Na sio kila mtu atakufaa kipindi unajiandaa na harusi yako au kipindi unatafuta mtu wa kukukopesha.
Pia, sio kila mtu atakufaa kipindi unaumwa au kipindi umefiwa.
Jambo moja tunalokosea ni kudhani kuwa yupo mtu atakayetufaa kwa kila kitu. Na kwa namna hiyo, tumepoteza watu wengi ambao wangekua na manufaa kwetu.
Anaekufaa kwa kila kitu ni Mungu pekee. Binadamu wote watakufaa tu kwa msimu.
Kinachotakiwa ni kutambua kila mtu anaekuzunguka anakufaa kwa nini, na kumtumia kwa hicho ambacho anakufaa.
Usivunje urafiki wa miaka mitano sababu tu hakuja kwenye msiba ulipofiwa. Ndani ya miaka mitano, hakukufaa kwa jambo jingine lolote lile?
Narudia, Chumvi haitakufaa kwa chai
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/chumvi-haitakufaa-kwa-chai-asubuhi-ila.html
No comments:
Post a Comment