Wednesday, February 5, 2020

UKIONA MWANAMKE WAKO AMEACHA KULALAMIKA KUHUSU MAMBO ULIYOKUWA UNAMFANYIA JUA KUNA

:
Fanya ujinga wako unavyoweza, lakini ukiona mwanamke ameacha kulalamikia mambo ambayo zamani ilikuwa ni kelele kubwa kati yenu basi jua kuwa kuna mambo mawili.
1) Jambo la kwanza inawezekana kuwa kashaanza kukuchoka na hajali tena.
2) Jambo la pili inawezekana ana mtu mwingine ambaye anampa amani, hata kama huyo mtu anajua hawawezi kuwa pamoja lakini angalau anafuraha kidogo na huyo mtu kuliko akiwa na wewe mume wake wa ndoa.
3) Jambo la tatu ni kwamba huyo mwanamke kashakukatia tamaa kuwa hutabadilika na kaamua kujipa furaha yake mwenyewe.
4) Jambo la nne wengi wakione wanawake zao wapo busy na mambo yao udhani wana mwanaume mwingine sio kweli, mwanamke akichukia anachukia kweli kweli. Unakuta wala hachepuki, na wala hana mpango wa kukuacha, wala hana mpango wa kutafuta mtu mwingine.
5) Jambo la tano husiombe mkeo au mpenzi akae ajiulize mambo aya:
1} Hivi nahangaika nini?
2} Nitapiga kelele mpaka lini?
3} Nitajibiwa matusi mpaka lini?
4} Nitahangaika na wanawake zake katika mitandao mpaka lini?
5} Hivi mimi ni mtu gani kila siku kupekua simu yake na kukuta mapicha ya uchi?
6} Hivi huyu mwanaume ni pumzi kwamba nisipohangaika naye nitakufa?
Ayo ni maswali mbaya sana mwanamke akijiuliza, sasa hole wako hapate jibu.
Kwaiyo naomba utambue kuwa ameacha kuhangaika na wewe na ameamua kujihangaikia. Ameamua kupendeza kwa ajili yake, ameamua kudili na maisha yake, kujifurahisha bila kujali kama umenuna au unaendelea na upuuzi wako!
Mwanamke akishachagua kuwa na furaha yake mwenyewe basi jua kuwa ni zamu yako ya kuteseka, ni zamu yako ya kukagua simu yake, ni zamu yako ya kupiga simu na kutuma meseji miamia kuulizia kuwa yuko wapi?
USHAURI WANGU:
Kama una mwanamke ambaye anakupenda sasa hivi, angalau anakuuliza kwanini unarudi saa nane basi mpende, mpe hata jibu zuri hata kama ni la uongo lakini acha kumtukana na kumdhalilisha.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/ukiona-mwanamke-wako-ameacha-kulalamika.html

No comments:

Post a Comment