Thursday, February 6, 2020

Tukumbushane mambo mbalimbali ya muhimu katika ndoa.

Image may contain: 2 people, people standing

1. πŸ’žMaisha ya ndoa siyo mkataba bali ni maisha ya agano kati ya mume na mke. Katika agano hili kila mmoja anahaidi kumpokea mwenza wake katika hali yake halisi.

2. πŸ’žMaisha ya ndoa ni safari ya kuvumiliana na kuchukuliana katika changamoto mbalimbali.

3. πŸ’žMaisha ya ndoa ni maisha ya kushirikishana kila jambo na mwenza wako. Mume wako au mkeo ndiye anayetakuwa kuwa rafiki yako mkubwa ambaye upo kumwambia lolote like.

4. πŸ’žMaisha ya ndoa yanajengwa kwa njia ya ukaribu wa mawasiliano ya mume na mke. Wanandoa tunatakiwa kuwa wawazi kwa kila jambo. Siri yoyote isiwepo katika maisha yenu.

5. πŸ’žMaisha ya ndoa ni maisha ya kuombeana. Hakuna jambo la muhimu kama kusali pamoja wanandoa na pia Sala ya familia. Usiwe mwenza ambaye wewe ni kinara kutoa sababu ya kukosa sala kila siku.

6. πŸ’žMaisha ya ndoa ni maisha ya kufindishana na kuelimishana. Kuishi pamoja ni kushirikishana vipaji vyenu na hivyo mnakamilishana, tuwe na unyenyekevu wa kukubali kujifunza.

7. πŸ’žMaisha ya ndoa ni wito wa kusameheana pale ambapo mmekoseana. Msikubali kulala na kinyongo moyoni mwako. Unapoweka hasira juu ya mwenza wako usiku kucha asubuhi maana yake hakuna salamu. Hali ya namna hii inavunja msingi ya upendo.

8. πŸ’žMaisha ya ndoa hayawezi kukwepa migogoro. Jiulize namna kwa mnakuwa na migogoro mnasikilizana kwa utulivu na siyo kununiana au kumdharau mwenza wako. Hakuna mkamilifu, migogoro yoyote ikitokea ni jambo la pamoja kurekebishe MSILAUMIANE.

9. πŸ’žMaisha ya ndoa ni muunganiko wa familia mbili. Familia ya mume na ya mke. Familia hizo kwa maisha yenu ya pamoja zinamekuwa familia moja hivyo mnapoamua kusaidiana katika mambo mbalimbali ndugu zenu mfanye kwa busara na hekima bila upendeleo wowote.

10. πŸ’žMakubaliano yenu katika ndoa yaheshimiwe na kila mmoja. Ndugu zenu wasiwayumbishe katika maisha yenu. Nanyi pia jambo ambalo mmejadili kwa pamoja siyo unaenda kwa ndugu zako unaliongelea kisha unaanza kumsemwa au kwenda kinyume na mwenza wako.

11. πŸ’žKila jambo msisimame pamoja. Nyie ni Wanandoa hivyo isionyeshe kupingana hasa kwa ndugu, marafiki au majirani. Usikubali ndoa yako kuzalauriwa maana ikitokea hivyo pia mnakaribisha maadui wa ndoa yenu.

πŸ’•❤️MUNGU AWABARIKI WANANDOA KATIKA SAFARI YA MAISHA YA NDOA❤️πŸ’•


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/tukumbushane-mambo-mbalimbali-ya-muhimu.html

No comments:

Post a Comment