✍ Kuna watu mmeumizwa na Mahusiano kiasi kwamba mnahtahi ushauri wa kusaikolojia ili kuyarudisha maisha yenu kama yalivyo mwanzo, ili muweze kupata imani mpya na mitazamo mipya juu ya mahusiano na kupata utahayari wa kufurahia mahusiano,
Na watu wa namna hii ni wengi sana katika makundi yetu haya ya whatsapp na huo ndo msaada unaowafaa na sio kuhtaji kumjua mtu sahihi wala asiye sahihi kwasababu tatizo mnalo ninyi wewe hivyo kuenda kutafuta mtu sahihi ni kuenda kumchafua mtu sahihi, maana tatizo umelibeba wewe
Na zipo dalili nyingi za watu wanahtaji msaada kama huo kuliko huu wa ushauri wa kimahusiano, na Endapo MTU atapatiwa msaada wa aina hii anaweza kubadilika sana na kuwa kiumbe kipya, mchumba mzuri, mama bora n.k
Kuna MTU ni single mom, anashindwa mpaka kumlea mwanaye, je MTU huyu anayeshindwa hata kumlea mwanaye unadhani akipata mwanaume sahihi atamfurahia?
Je tatizo ni yeye au ni MTU mwingine?
Je tatizo ni yeye au ni MTU mwingine?
*Jichunguze na Ujitambue ni msaada upi unaouhtaji*? *sio kuumizwa na mahusiano ndo ukimbilie ushauri wa mahusiano tu*
Na *Ukiona kila siku unapata masomo na unaomba ushauri lakini bado havikusaidii jua tatizo huhtaji ushauri wa hivyo, Bali ushauri wa saikolojia na sio huu wa kimahusiano*
Ushauri wa kisaikolojia ni unashauriwa namna yote ya maisha yako unavyoyaendesha na kutambua Thamani yako na kuwatendea wengine, ndipo utajijua ulivyo na kuanza kuishi maisha sahihi, kwani huezi kuwa na mahusiano sahihi ikiwa mwenendo wako wa maisha una walakini
✅✅
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/sio-kila-matatizo-ya-mahusiano.html
No comments:
Post a Comment