Saturday, February 8, 2020

MWANAMKE ! ACHA KUJIPANGIA MAISHA, MUDA WA MUNGU NI BORA ZAIDI KULIKO MATAMANIO YAKO!


Uyu mwanamke ana umri wa miaka 60, na ameolewa kwa mara ya kwanza maishani mwake.
Naweza kumwita Bibi au Shangazi yangu, ni Mama ambaye hajawahi kupata bahati yakuolewa usichanani kwake mpaka anaingia uzeeni, lakini hakukata tamaa aliendelea kumtumikia MUNGU kwa uaminifu katika kanisa moja la TAG pale Makongolosi Chunya.
Na wakati ulipo wadia akaja mume ambaye aliandaliwa na MUNGU, Felix Mwashitete, akamuoa nakufunga naye ndoa yakifahari kabisa. Sawa hawawezi kupata watoto kwa sasa, lakini katimiza ndoto yake yakuolewa nakufunga ndoa yakiroho.
Wengi wenu mtabisha kwamba mwanamke wa miaka 60s hawezi kuolewa, lakini tazama Lukia kaolewa kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yake tena kwa ndoa kubwa na ya aina yake.
Hii inaonyesha hakuna lisilo wezekana kwa MUNGU ukiwa na IMANI.
MUNGU ufanya kazi yake.
Na wakati Wake.
Na njia zake.
Kama umependa mpe:
"Hongera Shangazi Lukia"
___MAOMBI YANGU KWAKO___
Hongera kwa wote mnaoitwa wazee mtaani kwenu, maana naiona ndoa yako ukifunga na mtu sahihi kabisa kama MUNGU alivyo panga iwe, katika jina la YESU AMENI
Image may contain: 2 people, people standing, flower and wedding


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mwanamke-acha-kujipangia-maisha-muda-wa.html

No comments:

Post a Comment