Friday, February 7, 2020

MUNGU SIMAMISHA DUNIA NISHUKE


Hofu ya kusomesha, mchumba, mpenzi, mke inapotanda
Judy: umenipa ujauzito mpaka sasa sina matumanini ya kusoma tena, umenipotezea ndoto zangu Edgar.
Edgar: Sio hivyo Judy nakupenda sana na licha ya kwamba mimi ni mkulima nipo tayari kukusomesha mtoto akikua.
Judy: Wengi waliahidiwa hivyo na zikabaki kuwa ndoto walizo tembea nazo kila walikoenda.
Edgar: Naufahamu uwezo wako darasani tangu unasoma, siwezi kukubali ndoto zako zikapotea.
Hatimae Julieth akajifungua japo mtoto alifariki kwa bahati mbaya lakini, maisha yaliendelea huku Judy na Edgar wakiendelea na hughuli za kilimo na Ufugaji. Siku moja wakiwa shambani.
Edgar: Upumzike mwaka huu, mwakani urudi shule maana umri nao unaenda japo uzuri wako unanitishia usalama wa penzi letu.
Judy: Hofu yako tu, Mungu aliniumba na uzuri huu kwa sababu yako. Vile unavyoniona nakuvutia ndivyo nami unanivutia mpenzi wangu.
Edgar: Wengi walisema hivyo na maisha yao yamebaki kuwa historia, ule msemo wa ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima umegeuka siku hizi wanasema ukimsomesha mwanamke ni sawa na kulima shamba la miwa karibu na shule ya Msingi.
Judy: Hahaha!! Usinichekeshe Bhana, nakuahidi Mpenzi nakupenda sana na sitokusaliti.
Kwa kuwa Julieth alikuwa na uwezo mzuri Darasani alisoma elimu ya Kidato cha Kwanza hadi cha nne ndani ya miaka miwili na miwili aliitumia kwa utulivu kusoma kidato cha Tano na cha Sita tahasusi (Mchepuo wa PCB)
Alikwenda China kusomea udaktari miaka mitano baada ya kupata ufadhili, lakini kilichotokea hukoooo!!
Ulimbukenbi wa nchi za nje ukamjia.
Akasahau ahadi zote alizozitoa na kwa bahati mbaya alikutana na mtanzania mwenzake, Brown kijana mtanashati na aliyetoka familia tajiri akamchanganya.
Judy aliendelea kufanya vizuri darasani, lakini hakumkumbuka tena Mpenzi wake Edgar.
Mara awasilianapo nae humkatisha na kumwambia yuko Discussion, anasoma, anajiandaa na mtihani, amelala, amechoka anahitaji kupumzika na kila aina za sababu ambazo zingemfanya tu asiwe na ukaribu wa mawasiliano na Edgar.
Edgar akawa mtu wa kuwaza juu yay ale mashamba aliyouza na mifugo yake ili mkewe apate walau mazingira safi na salama ya kuanzia chuo.
Akawaza gharama alizomsomesha, lakini bado aliendelea kumkumbuka na kumjulia hali japo wakati mwingine ilipita wiki Judy pasipo kujibu ujumbe wake.
Judy alipata ujauzito wa Brown akiwa masomoni na kubahatika kuza mtoto wa kiume.
Hatimae alimzaliza masomo yake na kuamua kurudi nchini. Sijui kama alitaka kumuumiza Edgar au hakukusudia ila kwa ufupi alimtaarifu juu ya tarehe ambayoa angerudi nchini, na hivyo kumsihi ampokee uwanja wa Ndege.
Edgar alialika rafiki zake na jamaa kutoka kijijini hadi Dar, akiwa na bashasha kubwa ya kumpokea mpenzi wake akiwa Daktari wa Upasuaji.
Ndege ilitua na mmuda wote macho ya Edgar yalikuwa katika kumuangalia mrembo akishuka.
Alimwona Judy kapakata mtoto mzuri wa kiume pembeni akiwa na kijana mwenye miraba minne aliyeonesha wazi ndiye mmiliki wa Judy.
“We finally arrived safely” aliongea Brown akismaanisha hatimaye tumefika salama na kumbusu Judy.
Edgar aliyashuhudia yote yale.
“Brown huyu ndiye Ex wangu anaitwa Edgar niliyekuambia tukiwa masomoni, Edgar karibu usalimiane na mume wangu Brown na Baba wa mtoto wangu” Alisema Judy
Edgar alijibu, Eeeh Mungu simamisha dunia nishuke mimi” Machozi ya kumbubujika mbele ya umati ulikokuja kumpokea mkewe.
SHARE


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/mungu-simamisha-dunia-nishuke.html

No comments:

Post a Comment