Sunday, February 9, 2020

Barua Ya Wazi Kwa Kijana Wa Kitanzania(kama una miaka kati 20 mpaka 30 soma hapa)


Hakuna kipindi kigumu kwenye maisha ya mwanadamu kama muongo wa tatu wa maisha yaani kati ya miaka 20 mpaka 30. Huu ni wakati ambao una changamoto nyingi sana za maisha na ni wakati ambao unaweza kujenga au kubomoa maisha yako moja kwa moja. Kama wewe upo katika kipindi hiki endelea kusoma hapa ili uweze kupata mwanga pale mambo yanapokwenda usivyotarajia. Kama umri wako umezidi hapo unaweza kusoma pia na ukawashauri wadogo zako au watoto wako. Na hata kama umri wako uko chini ya hapa sio vibaya ukajifunza na kujua ni nini unakwenda kukutana nacho mbele.
Huu ni wakati mgumu sana kwako.
Kwa maisha yetu ya kitanzania, kijana wa miaka kati ya 20-30 anakuwa anaingia elimu ya chuo, yuko chuoni, amemaliza chuo, anatafuta kazi au ndio ameanza kazi. Pia ni wakati ambao kijana huyu anakuwa kwenye mahusiano ya mapenzi, uchumba na hata kuingia kwenye ndoa. Pia ni wakati ambao wengi wanaondoka kwenye mikono ya wazazi au walezi na kwenda kujitegemea wenyewe. Mambo yote haya yameleta changamoto kubwa sana kwa kijana na kwa changamoto hizi kijana anaweza kujijenga au kujibomoa.
Changamoto kubwa anazokutana nazo kijana katika wakati huu ni;
1. Kumaliza elimu ya sekondari na kwenda kuanza maisha ya tofauti kabisa vyuoni. Kuna tofauti kubwa sana ya elimu ya sekondari na elimu ya chuo, wakati sekondari unasimamiwa sana, chuoni unakuwa na uhuru zaidi. Kwa uhuru huu vijana wengi wamejikuta wanafanya mambo ambayo yanasababisha washindwe kufatilia masomo yao vizuri.
2. Kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuvunjika kwa baadhi ya mahusiano. Mahusiano sio rahisi katika umri huu, kijana anakutana na mwenzake ambaye anafikiri wanapendana sana na siku moja watakuwa mume na mke baada ya muda anagundua mtu aliyeingia nae kwenye mapenzi hakumjua vizuri. Hii inapelekea mapenzi kuvunjika na kuumizwa sana.
3. Kukabiliana na maisha ya masomo vyuoni na maisha mengine ya kijamii. Licha ya.....usikose!!!!


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/barua-ya-wazi-kwa-kijana-wa.html

No comments:

Post a Comment