Kama mpenzi wako hakujali, kila leo ni maumivu, kero na karaha na ukizingatia hujafunga nae NDOA jiongeze na achana na huyo haramia kabla maumivu hayajageuka kuwa majuto ya milele. Unawezaje kuvumilia mahusiano ya mateso na mtu ambae hata kwenu hatambuliki? Ukweli ni kwamba kuna baadhi ya watu wanahangaika na ndoa zao huku wakitamani kuchomoka kwa sababu walikuwa na mahusiano ya hovyo kabla ya ndoa na wakiwa na matumaini kwamba ndoa ndio itakuwa njia pekee ya kumbadilisha mtu na kuwa ktk mstari ulionyoka. Ndoa sio chuo cha mafunzo. Ndoa haimbadilishi mtu, ndoa huibua tabia halisi za mtu. Mahusiano kabla ya ndoa ndio chuo cha Mafunzo, ukimuona mwenzio haelewi somo, leave him/her for good...Ondoa hiyo oil chafu, subiri oil safi. Ndio maana nasisitizia sana umuhimu wa dhana ya mahusiano bora.
Kuna wakati yatupasa kukubaliana na hali halisi.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/02/acha-kuvumilia-maumivu-kwa-kigezo-cha.html
No comments:
Post a Comment