Tuesday, March 24, 2020

UNADHANI NI KWANINI WANAUME HUUMIA KWENYE MAHUSIANO/NDOA NA WASIWEZE KUSEMA?

Image may contain: one or more people, people sitting and indoor
Kwanza kwa uhalisia Mwanaume ndiye anae mtongoza Mwanamke, Kwa hivyo Mwanaume huamini baada ya kuachwa/kuacha atampata mwingine, Tofauti na Mwanamke ambaye yeye anatongozwa ndo maana wanawake akiisha ingia mahala kutoka sio rahisi, Pili Wanaume kuumizwa na wenza wao na kunyamaza ina majibu kwamba "WAO NDO CHANZO CHA HAYO ANAYOUMIZWA NAYO AMA MWENZA WAKE KUICHOKA TABIA YAKE" Mara nyingi ama kwa uhalisia wanawake ni watii sana kwa waume zao na hilo hawajifunzi ila ni kwa uhalisia wao, Utii ukizidi huleta woga na kila aogopaye hujihami, Mwisho wa mtu mtii ni KUJITETEA... Ndo maana mwanaume anapokuwa amegunduwa mwenza wake anamtendea ubaya hujua chanzo cha hayo maana hujua ni SEHEMU YA MALIPIZI! Kushindwa kusema kwa wanaume kwa yale wanayapitia kwa wenza wao ni wazi wanakosa UJASIRI kutokana na yale waliyowatendea wenza wao huko nyuma, Wanawake ni wepesi kusema wanayoyapitia kwa sababu wao huishi na wenza wao kwa UTII na hilo ndilo huwapa ujasiri hata wapaze sauti zao, MTENDA AKITENDEWA HUHISI ANAONEWA.
#Elista_kasema_ila_sio_sheria ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/unadhani-ni-kwanini-wanaume-huumia.html

No comments:

Post a Comment