Monday, March 30, 2020

WANAWAKE NI WAVUMILIVU SAANA ILA MOYO WAO UKITOKEA KUKUCHUKIA KAMWE USITEGEMEE MWANAMKE AKARUDI NYUMA NDO MWISHO WA UVUMILIVU WAO๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚


Mwanamke akikupenda, lazima atakuvumilia kwa kila jambo, hadi kwa mambo yako yasiyofaa, yanayomkera, yanayomuumiza na kumtesa kihisia.
Kutokana na ufinyu wako wa akili, utaendelea kumtesa na kumfanyia vituko kila kukicha huku ukidhani kuwa hawezi kukuacha, na hata akikuacha lazima atakurudia baada ya siku kadhaa, yani hawezi kuishi bila wewe.
Kaka zangu uvumilivu una kikomo chake.
Na usiombee mwanamke wako afikie kikomo chake cha kukuvumilia.
Utakuja kujuta, sababu mwanamke akifanikiwa kumove on, huwa harudi tena nyuma.
Akishakutoa moyoni, huwa hawezi kukurudisha tena.
Tabu itabaki kwako ukisota kumrudisha tena kwenye himaya yako.
Kama unampenda, basi acha kumfanyia vituko, acha kumtesa kihisia,acha kumnyanyasa,acha kumuonyesha vicheche vyako na pia acha tabia ambazo zinamkera mke wako Au mchumba wako.
Jifunze kumjali na kumthamini kabla hajaondoka kwenye maisha yako.
Utakuja kupoteza kuruka majivu na kukanyaga moto!!!!!! Tambua maumivu ya penzi yanauma saaaaanaร aa

Image may contain: 1 person


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/wanawake-ni-wavumilivu-saana-ila-moyo.html

No comments:

Post a Comment