Friday, March 27, 2020

HII NI KWA WANAWAKE WOTE AMBAO HAWAJAOLEWA.



Bootilicious Tanzanian model Sanchoka shows off wads of cash on ...
zingatia haya.
Kama wewe ni mwanamke na haujaolewa na upo kwenye mauhusiano na mwanaume ambaye haujafunga naye ndoa basi zingatia hili, linaweza kukusaidia na kukupa nuru nzuri ya ndoa bora yenye tija katika maisha yako ya mauhisiano.
Chagua mwanaume bora kwa kutizama utashi wake na mawazo yake chanya, mwanaume bora ni yule aliyekuzidi utashi, tabia nzuri pamoja hekima na busara na mwenye mapenzi ya dhati kwako.
Mwanaume anayekufaa ni yule anayekujali na kukuheshimu, mwanaume bora ni yule anayekupa mawazo ya kesho akiwa leo, mwanaume anayekufaa ni yule anayekufuta machozi na asiyekuliza kila siku.
Dada yangu tafuta mwanaume ambaye ni kichwa ili wewe uwe shingo sababu hakuna kichwa pasipo shingo.
Tengeneza mwanaume wako bora, anza naye kwenye maisha ya chini mkipeana faraja na matumaini ya kutengeneza ndoa bora na yenye mafanikio ya kipesa, na mahusiano yenye afya yaliyo na mapenzi matamu na bora, usipende wanaume wa wanawake wenzio mtengeneze handsome wako.
Dada yangu achana na mabrothermen wanaopaka poda, wanawanaotembea na selfiestick hawana tija, mwanaume bora havai mlegezo.
Mwanaume bora hata kama hana pesa daima huwa na hazina ya mawazo na ndoto zenye matumaini ya kuwa na future nzuri baadaye.
Achana na wanaume maarufu wengi wao hawana mapenzi ya dhati wanapenda kuwatumia wanawake kwa tamaa zao za mwili.
Dada yangu mimi nakupenda na natamani uwe na ndoa bora na uchague mpenzi bora, mpende mpenzi wako kwa moyo wote achana na zile kauli za wanaume wote wanafana.
Muombe Mungu akupe mume bora na wewe uwe mke bora sababu mke mwenye mapenzi ya dhati huwa anabeba baraka za mafanikio ya mume wake.
Tafakari mauhusiano yako yapoje.
Wakati ni sasa sio kesho acha kuwa na idadi kubwa ya wanaume, chagua mwanaume wako mmoja bora, pia achana na utamaduni wa kuchat na wapenzi wako wa nyuma.
Tengeneza mume wako bora achana na wanaume wadhaifu na wasio na tija kwako chagua wanaume bora kwa sifa za ndani na sio kwa ubora wa nje.


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/hii-ni-kwa-wanawake-wote-ambao.html

No comments:

Post a Comment