Saturday, March 28, 2020

EPUKA MAMBO HAYA UNAPOTAKA KUOA AU KUOLEWA:


Unapokua umefika umri wako wa kuhitaji mke sahihi au mme sahii wa ndoa yako, Hakikisha unatengeneza mazingira ya wew binafsi kwanza kuonekana mume mtarajiwa au mke mtarajiwa. Kuna mambo ya kuepuka endapo unataka kuoa au kuolewa.
๐Ÿ‘‰Jambo La kwanza la kuepukana nalo ni Aina ya maisha unayoishi. Mwanaume Unapokua katika harakati za kutafuta mwenzi au mwanamke unaposubir kupata mwenzi, Kuna aina ya maisha ambayo unatakiwa uyaepuke ila ukae katika mstarii sahihi. Mwanaume unapokua kweny process za kuchumbia ukimaanisha unahitaji mwenz wa ndoa sio na girlfriend, kuna makundi ya kihuni unatakiwa uyaepuke, makundi ya vijiweni kupiga soga zisizo na mpango au maendeleo, unatakiwa kuepuka maisha ya kivulana kuongozana na vijana wa mtaani, maana mwanamke unatayekua unamuhitaji huenda akiona aina ya maisha yakk ndio hiyo hutampata tena, na utakua unajiwekea pini mwenyewe. Mwanamke unatakiwa nawe uepukana na mashost wasio na mawazo chana, makundi yasiyojishulisha, kwepa vikundi vya umbea na usengenyaji. Hii itakusaida kuaa kweny sifa nzuri kipindi unachumbiwa. Usilalamike tuu kwamba huolewi angalia maisha unayoishi kwanza jee yana kigezo cha kuwa mke wa mtu.
๐Ÿ‘‰Jambo la pili la kuepukana nalo ni Aina ya mavazi unayovaa na mwenendo wa taiba yako kwa ujumla. Mwanaume Kuna aina ya mavazi ambayo unavaa yan hata ukimsogelea mwananke anakushangaa, mavazi ya kivulana yaepuka kabisa hii kuvaa milegezo hereni n.k epukana na aina hiyo ya mavazi. Unapotaka kuoa ni dhahiri umekua mtu mzima ebu onyesha utuuzima wako katika uvaaji na tabia zako, Ebu vaa mavazi ambayo hata ukimsogelea mwanaume anasema yes huyu ndiye mume niliyemsubiri kwa muda. Mwanamke epuka mavazi ya kuonyesha maungo yako, unaweza ukaniambia kuna wanaume wanapenda hivyo, Laah! Kubali mwanaume mmoja ndio apende uvaaji wako, yeye kama mmeo ebu jiweke vizuri then ukiolewa ndio akwambie napenda uvae vazi hili. Aina ya mavazi tuu inaakisi tabia yako epukana na mavazi ya uchi mwili wako ni mali ya mtu mmoja.
๐Ÿ‘‰Jambo la tatu la kuepukana nalo ni Uhongaji na Tamaa. Mwanaume unapochumbia Epukana na jambo la uhongaji wa fedha kwa mwanamke, usionyeshe kununua upendo kwa mwanamke ebu kama hakutaki pasipo pesa achana nae. Tabia ya uhongaji inaweza kukujengea taswira mbaya kuelekea maisha ya ndoa mwanamke anaweza kuona unayojeuri ya pesa hivyo unaweza kuhonga yeyote nje na akawa mali yako, Ebu tanguliza upendo wa dhati onyesha upendo wa kweli kwanza.
Nuhu mshauri wa mahusiano


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/epuka-mambo-haya-unapotaka-kuoa-au.html

No comments:

Post a Comment