Huna jema wewe kila kitu unalaumu tu, jana mkeo kazidisha chumvi kwenye mboga umemlaumu tena kwa vijimaneno ambavyo haviwezi kumfanya mtu ajisikie vizuri, leo kapika chakula kizuri na viungo kibao kaweka ili kuongeza ladha ya chakula humpongezi kwa chochote unakula kimyakimya au unatafuta kitu kingine cha kumtoa kasoro. Mumeo akichelewa unalaumu akiwahi kurudi unalaumu hata kidogo tu yani ili mradi tu wewe ni baba/mama lawama.
Hujui kuchukulia mambo katika mtazamo chanya wewe ni bingwa wa kutafsiri vibaya.akisema hivi wewe unatafsiri hakutaki tena, ukipiga simu isipokelewe unawaza tayari anakusaliti,mahusiano mengi yanakufa kwasababu tunashindwa kuwawazia vizuri wapenzi wetu tukidhani labda ndio njia nzuri ya kuwatuliza kumbe ndio tunawakimbiza.
Fikiria mnaishi wawili tu halafu unajifanya kutafuta pesa fulani ukidai uliiweka kwenye meza ya chumbani kwenu "Kweli tena .niliiweka hapa mezani sasa nani kachukuwa??" Unataka mwenzio ajisikie vipi!? Yeye ndio kakuibia sio?? Chunga bakuli lako angalia unaongea nini na kitaleta athari gani kwa mwenzio!
Usiwe mtu wa kupokea tu katika mahusiano yenu ukadhani jukumu la kupenda sio lako ni lakwake, yeye ndio akubembeleze wewe, akununulie zawadi, akupigie simu, akutumie msg tena asipofanya hivyo unalaumu. jaribu kutafuta namna ya kujibu mapigo ili penzi liwe na amshaamsha vinginevyo huwezi kuishi na mtu yeyote mahusiano yatakufia mikononi kwa vijitabia vyako vya chinichini ambavyo sio siri ni vidogovidogo ila vinaboa sana!...BADILIKA
Like
Share
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/ukiwa-mtu-wa-namna-hivi-mahusiano.html
No comments:
Post a Comment