Monday, March 30, 2020

NDOA NI KUJITOA SADAKA + UVUMILIVU


Kuna kijana alikua anajua kuwa mke wake anatoka nje ya ndoa basi akamwuliza mke, mkewe akakataa, akamwambia baba yake akaambiwa na babaake tulia mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku analalamika kwa
babaake, mwisho babaake akamwambia basi ntakusaidia. Itabidi ujifanye unaumwa sana hoi
hujiwez halafu nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya anaumwa mzee akaitisha kikao cha ndugu wote pande 2, Mzee akaanza kueleza jaman kijana wetu anaumwa amepata ugonjwa wa utata hospital zote umeshindikana hivyo tumeenda kwa mganga wa jadi amenipa dawa na ina masharti, inatakiwa atakaye iandaa hii dawa awe mwanamke mwenye ndoa ambaye hajawah kutoka nje ya ndoa tangu alipoolewa ndo kijana wetu atapona! Kama ametoka nje ya ndoa asiandae dawa hii kwa sababu tukimpa kjana wetu watakufa wote! Je kina mama nani
ataandaa? Walitoka nje wamama mmoja mmoja hadi mkewe na mamake mzazi wakatoka, akafata mama ake kijana, mashangazi na dada zake, mwisho wakabakia wanaume peke yao! Mzee akamwambia mwanangu umeona hali za
ndoa zilivyo? Acha kujisumbua tulia na
mkeo nadhani umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜…
Like
Share

Image may contain: 1 person


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/ndoa-ni-kujitoa-sadaka-uvumilivu.html

No comments:

Post a Comment