Miujiza huanza kutokea pale ambapo unaielekeza akili yako katika ndoto zako na si katika uoga. Najua kua mara kadhaa ushapanga kufanya jambo flani, unahamu, ni kitu cha ndoto yako.
Lakini kila mara ukitaka kufanya kitu hicho kunakuwa na uoga flani, inaweza kuwa labda sitapata wateja, labda ntashindwa kufanya hivi, watu watanichukuliaje na vitu kama hivyo.
Unaogopa na hutaki kabisa kufanya kile kitu. Unakata tamaa na muda unaenda, unaacha uoga unashinda na mara kadhaa unaanza kulalamika kuwa Mungu hajanibariki, unasema kwanini mimi unalia kabisa.
Unajiona mpweke na kujiona mwenye mikosi. Lakini huna mikosi bali uliacha uoga ukashinda. Kuna mambo mengi unaweza kuyafanya kama ukiamua kuangalia mbele, ukaweka uoga pembeni na kufuata ndoto zako.
Hembu acha kuangalia changamoto sasa, acha kuangalia mambo ambayo unahisi yatakukwamisha na kuanza kuangalia mambo ambayo unahisi yatakusaidia kufanikiwa.
Kuangalia changamoto kabla ya kuanza kufanya kitu flani kutakusababishia kuacha kabisa kukifanya kile kitu kwa hofu ya kushindwa, kuangalia changamoto ni kushindwa kabla ya kuanza.
ππππππππππππ
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/acha-kuruhusu-uoga-ushinde.html
No comments:
Post a Comment