Tuesday, March 31, 2020

HIVI NDIVYO MKE ANAVYOWEZA KUSABABISHA MUMEWE KUTEMBEA NA HOUSEGIRL

Irene Uwoya loydemich
Kabla hujamlaumu mume kwa tabia aliyoianza ya kumtafuna housegirl au michepuko ni vema mwanamke kama mama wa nyumba ukajitafakari kiwango cha huduma yako kwa mmeo ndani ya nyumba isijekua wewe ndio chanzo. Mwanamke asiyejua wajibu wake mara nyingi huwa chanzo cha mume kumtafuna housegirl mfano Tafakari hapa:
MUME: darling ninakikao mkoani kesho
naomba niandalie vitu please
MKE: dada zile nguo za baba pamoja na soksi ulifua?
DADA: ndio nimepanga kabatini. Mama anarudi chumbani na
kumuomba hubby wakacheki TV
sebulen, lakn baada ya muda mama
anamuita dada akapange suruali
kadhaa na mashati kwa ajili ya safari
ya kesho, dada anapanga kila kitu anatoka. MKE: kama tayari hakikisha
unarekebisha yale mashuka pale
kitandan weka na maji bafuni. Dada anafanya na kwenda zake
kulala, asubuhi dada anaamka
mapema na kuandaa kila kitu
ikiwamo na chai, baba anakunywa
chai na kutaka kuondoka. MKE: dada msindikize baba ili ufunge
geti sbb bado ni giza
DADA: sawa mama. Dada anatoka na begi la baba hadi nje
kwavile mkewe yupo ndani, baba
anamtaka dada abaki vizuri na
watoto, dada anaitika na kusema
nawao wanamuombea safari njema.
Baada ya muda baba anarudi toka safari. MKE: huku akitabasam, dada si
umemuona baba amerudi vipi chakula
tayari?
DADA: ndio.
MKE: haya kapange meza vizuri mimi
nandaa juice. Baada ya muda wanakula na baba
anagundua juice sio nzuri anaamua
kuiacha na kusema leo wamesahau
kuweka baadhi ya vitu hivyo
hataweza kuinywa. Baadae baba
anakumbuka kuwa aliacha boxer zake kwenye ndoo ya maji chumban
na kufunika mfuniko, anamuuliza
mama vipi zile nguo zangu kwenye
ndoo zilifuliwa? Maana nilisahau
kusema kama zina maji. MKe: dada njoo hapa hivi zile nguo za
baba chumbani ulifua?
DADA: ndio mama (lkn hasemi kama
alianua na kuweka chumbani kwake
akidhan atakunja baada ya kazi
kupungua) MKE: darling zilifuliwa.
MUME: na watoto vipi wameshalala?
MKE: anajibu wamelala darl.
MUME: vipi dereva wao alifika
kuchukua pesa yake?
MKE: dada eti uncle Hassan amechukua pesa yake?
DADA: hapana wamembadilishia gari
uncle Hassan amesafiri kwa muda. MKE: tutampatia darl siku akirudi acha
dada aendelee kuitunza
MUME: basi vizuri, ehee vipi na tution
walienda leo
MKE: ndio walienda (anamgeukia
dada, si eti ee walienda si eti) DADA: hapana Kelvin anaumwa leo
siku ya pili nilinunua dawa dukan
nimempa lkn hajambo.
MKE: (anashangaa) heeE! mtoto
mgumu huyu kumbe jana alikua
mgonjwa halafu wala!!! alikua anacheza tu jamani watoto!! Asante
dada umefanya vizuri
MUME: haya mimi niwaache nataka
nikapumzike lkn darl nitaomba zile
boxer nichome kabla ya kulala
sababu zimeanza kuchoka MKE: anaingia chumbani anafungua
kabati na kuzikosa lkn kabla
hajajieleza anamuona dada analeta
mzigo wa boxer zikiwemo chupi za
mama na mataulo
MUME: basi dada zirudishe tutachambua kesho nenda kafanye
kazi zako. mume anainuka na kuelekea kulala,
lkn anagundua mke wake alimwaga
nguo kitandan wkt anatafuta boxer
hivyo anaamua kurudi sebuleni ili
aombe kuandaliwa kitanda, kwavile
chumba cha dada kipo jiran na chao anagundua dada ameacha mlango
wazi, anaamua kuufunga ili mbu
wasiingie lkn anaona baadhi ya
mashati na suruali zake zikiwa
zimenyooshwa na kuwekwa pemben
huku kitanda kikiwa kimetandikwa kwa ustadi anaamua kufunga mlango
na kutoka, anafika sebuleni anakuta
mama anatazama tamthilia
anamwambia akatandike kitanda. MKE: dada njoo, (kwa sauti ya
kunong'ona) naomba ukatandike
kitanda haraka
DADA: tayari nilipeleka viatu vya baba
nikaamua kutoa na zile nguo
MKE: anaamka na kwenda kuhakikisha anarudi na kumwambia
mumewe tayari aende akalale
MUME: anaenda kulala lkn huku
akijuiliza sana ni nini amfanyie huyu
dada kwa ukarimu anaowafanyia
hapo nyumban, kwanza anajua ni vitu gani baba anabeba akiwa safarini,
ndio pekee anaemtakia safari njema
na kumuombea, ndio anaefua boxer
zake na kutunza vizuri, ndio anaepika
chakula kitamu, ndio anaetandika
kitanda chake, ndio anaejua juice gani baba anapenda, ndio anaejua kama
watoto wamerudi vipi kutoka shule,
vilevile ndio anaejua kama watoto
wake wanaumwa ama vipi. Sasa mnafikiri baba atamzawadia nini
huyu binti ambae amebakiza kujua
style anazopenda baba tu, si
atamfundisha ili kesho asimsumbue
tena mke wake ambae kila kitu lzm
amuulize dada. Akina baba hawaridhiki lkn wamama jitahidini
hata kama mnamajukumu kiasi gani.tunajifunza nini wanawake wengi huwatengenezea wadada wa kazi mazingira ya kuvuruga ndoa zao bila kujituma sambaza ujumbe huu kwa wanandoa wote na wanaojiandaa kuoa na kuolewa


source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/hivi-ndivyo-mke-anavyoweza-kusababisha.html

No comments:

Post a Comment