Ingawa kukaa muda mrefu kwenye mahusiano na mwanaume hakumaanishi kuwa ni lazima ndoa yenu itakua nzuri lakini kua makini sana na wanaume ambao huja na harakaharaka za kuoa. Mwezi wa kwanza tu wa mahusiano ashaanza habari za kuoana. Tena sio wale ambao mnaanza mahusiano mnakua siriasi mnapendana ndiyo anataka kuoa, hapana wale ambao amekuona tu anakuambia nataka kukuoa ukimuambia sababu anakuambia sijui umri, mara kwetu wananisumbua au anataka mtoto.
Mnaweza kukutana watu mwezi tu mkapendana na kila mmoja akajisikia raha kuwa na mwenzake, lakini nikuambie tu mapenzi hata wewe mwenyewe utayajua na kulazimishia utakujua. Hataki ujue kweo, hataki umjue vizuri, hataki ujue mambo yake ya nyuma, ni msiri hata kwa marafiki lakini anataka kukuoa ghafla na mimba juu. Ndugu yangu kuwa makini, haiwezekani mtu mwenye munkari wa kuoa namna hiyo akakosa mke kwa haraka hivyo.
Kama hao wengine walimkataa basi jua kuwa kuna tatizo flani. Bado narudia kuna wale ambao wakati mnakutana hata ishu ya kuoa walikua hawana, walikua wanapita ila baada ya kuonga wakanogewa, hawa hawana shida sana, ila wale wanakuja na mizuka yao yakuoa, wanalazimishia kwamba hata kama ingekua nani wangeoa hawa kuwa makini nao kwani wengi wanakua vimeo. Kama ni kukuoa hata kama ni baada ya siku tatu basi ije otomatiki mjikute tu wote mnataka kuoana na si yeye amekuja na ndoa yake mkononi!
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/kukaa-kwenye-mahusiano-muda-mrefu.html
No comments:
Post a Comment