Sijui ni nani anataka kusikia hili. Lakini nikwambie tu, unapokuwa katika msimu wa upweke, kubaliana na hali. Mungu sio Muongo, wala si mwanadamu hata aseme uongo. Hawezi kukupitisha katika msimu wa upweke na maumivu bila kukuandalia njia ya kuchomoka. Hawezi kukutoa mahala ulipokuwa Ukidharauliwa, ulipokuwa ukijihisi huna thamani na ulipoteswa na kukuacha Njiani. Hawezi kukutoa Misri bila ya kukufikisha Kanani.
source https://utamuzaidiapp.blogspot.com/2020/03/sijui-ni-nani-anataka-kusikia-hili.html
No comments:
Post a Comment